MANJI ATUPA KOMBORA TFF, ASEMA HAWATAMWACHA MURO 'ANYONGWE', AELEZA KAMISHNA CAF KUSHAWISHIWA, AMVAA MALINZI KWEUPEE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
wiki chache zilizopita, kumekuwepo migongano mingi kuhusiana na masuala
ya klabu ya Yanga (Young Africans Sports Club) ambapo haikuwa vyema
kuyajibu au kuyajadili wakati klabu hiyo ilikuwa ikikabiliwa na
mashindano ya kimataifa. Lakini kwa hivi sasa ambapo mambo yametulia,
nimeona ni wakati mwafaka wa kuyaelezea kama ifuatavyo:
1. TAARIFA YA MCHEZO KATI YA YANGA NA TP MAZEMBE
1.1. Ningependa
kumshukuru Rais wa Shirikisho la Miguu wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye
amenipongeza nikiwa kama Rais wa Yanga kutokana na mafanikio
yaliyofikiwa na klabu hiyo katika mashindano ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika. Hata hivyo, ningependa kuanza kwa kuelezea kwamba mimi Si
Rais wa Yanga bali Mwenyekiti, na nikiwa Mwenyekiti wa Yanga, kwa niaba
ya klabu hiyo, ninazipokea pongezi hizo.
1.2. Hata
hivyo, pongezi hizo zingepokelewa kwa moyo mkunjufu zaidi na Yanga
iwapo TFF ingeisaidia Yanga kama inavyotakiwa kufanya. Mambo ambayo
TFF ingeyafanya na kuimarisha utendaji wa klabu hiyo ni pamoja na:
1.2.1. Kutoingilia
ratiba ya ligi kuu mwaka jana ambapo iliiruhusu Azam FC kufanya ziara
ambayo ilikuwa nje ya ratiba na hivyo kufanya mabadiliko katika ratiba
ya ligi, jambo lililotufanya kushindwa kujipanga vyema.
1.2.2. Ingetoa
mjumbe wa masuala ya kisheria kutoka TFF kwenda Yanga kwa ajili ya
mchezo wa marudiano wa klabu hiyo uliofanyika huko Angola ambapo ujumbe
wetu pamoja na wa vyombo vya habari, ulifanyiwa fujo na kupigwa na
polisi wa Angola. Matokeo yake, badala ya kutuunga mkono katika
kupeleka rasmi malalamiko yetu kwenda Shirikio la Soka la Afrika (CAF),
TFF lilikaa kimya.
1.2.3. Ilibidi
itupe vifaa vya CAF vilivyotumwa kwa ajili ya kutumika katika hatua za
makundi kwa wakati unaotakiwa, jambo ambalo halikufanyika na kutufanya
tuingie gharama ambazo hazikuhitajika na kutusababishia adhabu kutoka
CAF.
1.2.4. Ilibidi
ichukue hatua kutokana na kuonyeshwa kwa klabu yetu kadi nyingi mno za
njano (8) na kadi moja nyekundu katika mchezo wa kundi letu nchini
Algeria dhidi ya klabu ya MOB.
1.2.5. Ingehakikisha inatuonyesha
wazi tarehe na muda wa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP
Mazembe ambapo badala yake waratibu waliamua kuupanga mchezo huo dhidi
ya TP Mazembe dhidi ya maslahi ya Yanga. Hali hiyo ilizidi kuvurugwa
kwa kufikiwa mkataba wa siri na Azam TV wa kuurusha nchini Tanzania
mchezo huo wa Yanga wakati klabu ilikuwa imepiga hatua katika
majadiliano ya shirika la utangazaji ya TBC (ambao mwaka jana walikuwa
wamepokea magari matatu kutoka China ili kuimarisha matangazo ya moja
kwa moja ambayo yaligharimu kiasi cha Shilingi bilioni 5 kwa kila gari)
kwa ajili ya kwa ajili ya kiwango kinachotakiwa katika kurusha matangazo
kimataifa.
1.2.6. Pia
ilibidi kuipa Yanga fedha za CAF kwa kufuzu kuingia katika hatua hiyo
ya mashindano ambayo ilifahamika kuwa ni Dola 15,000 za Marekani; fedha
za Kombe la FA katika mchezo wake na Azam FC; Zawadi ya VODACOM ya Ligi
Kuu, zote hizo zikisemekana kuwa ni kiasi cha Sh. Milioni 500, ambazo
iwapo zingelipwa na TFF katika muda mwafaka, Yanga ingezitumia fedha
hizo kukabiliana na majukumu mbalimbali ya fedha ikiwa ni pamoja na
bonasi za wachezaji hadi usajili wa wachezaji katika dirisha maalum la
CAF, na kadhalika.
1.3 Mahali
ambapo klabu inasimama leo hii ni kutokana na juhudi zake yenyewe na si
kutokana na ushirikiano au msaada wowote ambao Yanga imeupata
kutoka TFF ambapo Yanga kamwe haikuutegemea na ambapo imeona waziwazi
kwamba TFF imeshindwa kuisaidia.
1.4
Uamuzi wa Yanga kuwaruhusu mashabiki wa soka kuingia bure katika mchezo
huo ili kuweza kumpata mchezaji “halisi japokuwa wa kufikirika” wa 12
si jambo jipya katika soka, japokuwa jambo hilo limekwenda kinyume na
matakwa ya TFF ambayo ilitegemea kufanya makato mbalimbali
ambayo yamefutwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Pamoja na hayo yote, kama TFF wanataka kusimamia michezo yetu, basi wachukue gharama zote za maandalizi kabla ya kwenda kwenye michuano kama nauli, posho za wachezaji na kadhalika, hesabu tutawapelekea hivi karibuni. Tunammsihi Rais wa TFF asigeuke kauli yake maana sisi tumewaachia kutafuta fedha kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazokuja kulingana na uzito, tunaamini hatageuka.
Pamoja na hayo yote, kama TFF wanataka kusimamia michezo yetu, basi wachukue gharama zote za maandalizi kabla ya kwenda kwenye michuano kama nauli, posho za wachezaji na kadhalika, hesabu tutawapelekea hivi karibuni. Tunammsihi Rais wa TFF asigeuke kauli yake maana sisi tumewaachia kutafuta fedha kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazokuja kulingana na uzito, tunaamini hatageuka.
Tunashangaa
CAF na TFF walikuwa wapi wakati rais mstaafu Jakaya Kikwete katika
mchezo wake wa kwanza katika Uwanja wa Taifa alipowaruhusu mashabiki
kuingia bure? Inabidi wafahamu pia kwamba tulipocheza huko Angola na
Algeria, mashabiki waliruhusiwa kuingia viwanjani bure tulipocheza
huko. Sisi kama klabu tunawathamini mashabiki wetu katika kututia
hamasa wakati tunacheza.
Mimi
mwenyewe nilitoa fursa hiyo huko Mwanza miaka ipatayo kumi iliyopita
wakati klabu ilicheza dhidi ya El-Merreikh, na hapakuwepo na adhabu
yoyote kutoka CAF kutokana na hatua hiyo. Je, TFF wanatufanyia hivi
kama kutuadhibu kutokana na kukosa mapato ambayo yangeliwezesha
kufanikisha sikukuu ya Idd el Fitri?
1.5
Uamuzi wa kuwaruhusu mashabiki kuingia bure Uwanja wa Taifa ni jambo
lenye busara nyepesi kufahamika kwa mtu yeyote. Katika mchezo huo ambao
ulipigwa uwanjani hapo, mapato yasingezidi Sh. 100 Milioni, na baada ya
makato yote ambayo yangehitajika kufanyika, klabu ingejikuta imebaki na
kiasi cha Sh. 40 Milioni. Hii ni kwa kuchukulia kwamba pasingefanyika
wizi wowote kwenye milango na pasingekuwepo na tiketi bandia, hali
ambayo hufanywa katika michezo ambayo husimamiwa na TFF hasa ile ya
ligi.
1.6 Binafsi
niliamua kwamba kwa vile Uwanja wa Taifa ulikuwa umekodishwa kwa ajili
ya maonyesho ya starehe kwa Sh. 20 Milioni ambapo kwa uelewa
wangu kiasi hicho kilikuwa kimefutwa na Waziri wa Michezo na Utamaduni
kwa kuwa Yanga ilikuwa inawakilisha taifa. Klabu iliona ingebeba gharama
zingine mbalimbali zenye kuhusika na mchezo huo, yote hayo kwa ajili ya
kutaka mashabiki wengi wa Tanzania waingie ili kuitia moyo Yanga katika
siku hiyo ya mchezo.
Niliongea
na vyombo vya usalama, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusu nia hiyo
ya Yanga, ambapo jeshi la polisi lilifanya kazi nzuri sana. Hali ya
uwanjani ilikuwa tulivu kabisa isipokuwa nje ambako baadhi ya mashabiki
waliuziwa tiketi feki ambazo tunahisi zilikuwa zimetayarishwa na
TFF. Hata hivyo, polisi waliweza kudhibiti hali hiyo ambapo hakuna
aliyejeruhiwa au kukamatwa, jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba woga wa
CAF wa kuiadhibu Yanga kutokana na kinachodaiwa vurugu, ni upuuzi
mtupu.
1.7
Kuhusu suala la kutakiwa mashabiki 40,000 pekee waingie katika uwanja
huo wenye kubeba watu 60,000, jambo ambalo lilizua sababu kutoka CAF
kuiadhibu kwa kuipiga faini Yanga, ninashangaa ni busara gani ilitumiwa
na serikali katika kujenga uwanja wa kuingiza watu 60,000 na badala yake
kutegemea uingize watu 40,000 tu!
Rais wa TFF hakupewa habari za kweli. Ninachofahamu ni kwamba mratibu wa mechi alisema kwamba maofisa wa TFF walitaka waingie watu 40,000 tu ili kuipunguza nguvu Yanga lakini alikataa, kwani hakuona sababu ya watu kuingia na kuujaza uwanja kama ilivyo kawaida.
Rais wa TFF hakupewa habari za kweli. Ninachofahamu ni kwamba mratibu wa mechi alisema kwamba maofisa wa TFF walitaka waingie watu 40,000 tu ili kuipunguza nguvu Yanga lakini alikataa, kwani hakuona sababu ya watu kuingia na kuujaza uwanja kama ilivyo kawaida.
Isitoshe, Kamishna
huyo ninaweza kumleta mbele ya Watanzania wasikie jinsi TFF ilivyokuwa
inajaribu kumpotosha dhidi ya Yanga kwa vile klabu hiyo ilikuwa imeamua
kuionyesha mechi hiyo bure na kuvinyima fursa vituo fulani vya
televisheni kuuonyesha mchezo huo, pamoja na kuvuruga mipango ya TFF ya
kupata fedha kutokana na mauzo ya tiketi. Katika hili, nina fahari
kubwa kwa kutoa fursa kwa zaidi ya mashabiki 60,000 kuiona mechi hiyo
bure ambayo hata kama hatukushinda lakini tulikuwa pamoja kama
Watanzania.
1.8 Nawajulisha
wananchi kwamba uhasama kati ya TFF na Yanga si mpya kwani hata katika
uchaguzi tuliofanya majuzi, kulikuwa na majaribio ya kutaka kuvuruga
matokeo yake, na njama hizi zimefikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Ni vyema TFF ikashughulikia matatizo yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga matokeo ya mechi mbalimbali, kuingilia masuala ya klabu mbalimbali kama ilivyofanywa kwa Yanga kwa kujaribu kutumia katiba ya zamani ya mwaka 2010, kuingia mikataba ya siri na wadhamini wa ligi, haki za vituo vya televisheni kuonyesha mechi na kusababisha kuziua klabu kifedha, na kujifanya kuchukua hatua za maendeleo katika soka kwa unafiki wa kutegemea kodi mbalimbali kutoka Yanga na Simba.
Sisi katika klabu ya Yanga tuliokuwa katika Kamati ya Utendaji hatuchukui hata posho za vikao kwani tunataka kwanza kuifanya klabu ijitegemee kifedha kabla ya maslahi yetu binafsi. Kinyume chake, posho ndani ya TFF limekuwa jambo la kawaida, hali ambayo imefanya hata mahesabu yake yasichapishwe kwa ajili ya kupitiwa waziwazi na kila mtu.
Ni vyema TFF ikashughulikia matatizo yake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga matokeo ya mechi mbalimbali, kuingilia masuala ya klabu mbalimbali kama ilivyofanywa kwa Yanga kwa kujaribu kutumia katiba ya zamani ya mwaka 2010, kuingia mikataba ya siri na wadhamini wa ligi, haki za vituo vya televisheni kuonyesha mechi na kusababisha kuziua klabu kifedha, na kujifanya kuchukua hatua za maendeleo katika soka kwa unafiki wa kutegemea kodi mbalimbali kutoka Yanga na Simba.
Sisi katika klabu ya Yanga tuliokuwa katika Kamati ya Utendaji hatuchukui hata posho za vikao kwani tunataka kwanza kuifanya klabu ijitegemee kifedha kabla ya maslahi yetu binafsi. Kinyume chake, posho ndani ya TFF limekuwa jambo la kawaida, hali ambayo imefanya hata mahesabu yake yasichapishwe kwa ajili ya kupitiwa waziwazi na kila mtu.
1.9
Nasisitiza kwamba katika uchaguzi uliofanyika majuzi, kabla ya hapo
nilikuwa Mwenyekiti nikiwa nimechaguliwa kwa kura kwa kipindi cha miaka
miwili katika uchaguzi mdogo nikiwa nimeapa kuleta uaminiano kati ya
mashabiki na viongozi wa klabu, ambapo kipindi hicho kiliongezwa baadaye
kwa mwaka mmoja na wanachama wa klabu, na kuongezwa tena kwa mwaka
mmoja kutokana na kufanyika uchaguzi mkuu mwaka jana kutokana na ushauri
wa maandishi wa TFF.
Nimesema
wazi kufuatia uchaguzi wa majuzi kwamba nitapigania maendeleo ya klabu
kwani hapatakuwa na cha kufurahia na kuleta amani na utulivu katika
klabu iwapo Yanga itashindwa kushiriki katika michuano ya soka barani
Afrika, jambo ambalo mashabiki wa Yanga wanalitaka siku zote.
1.10 Pia
ninanyoosha mkono wa urafiki kwa klabu ya Simba kwa uchaguzi wao,
japokuwa wao hawakufanya hivyo niliposhinda. Nimeelekeza kwamba utani
(ushindani) kati ya Simba na Yanga uwe katika viwanja vya soka, ndiyo
maana katika mechi yetu na TP Mazembe niliwakaribisha kama Watanzania
wenzetu, tuliwaheshimu wote pamoja na wale waliovaa majezi na
kuishangilia TP Mazembe.
1.11
Mkono huo wa kutakiana mema sitaki ubadilike na kuwa ngumi, bali
uendeleze ushirikiano, na TFF iache njama zake dhidi ya Yanga bali
iungane nasi katika kujenga soka la Tanzania.
2. KUITWA KWA JERRY MURRO KATIKA KAMATI YA MAADILI YA TFF AKIWA MKURUGENZI WA HABARI WA KLABU
2.1. Hati
za TFF za kuitwa kwa Jerry Murro hazionyesha wazi sababu ya Mkurugenzi
wa Habari huyo wa Yanga kutakiwa kufanya hivyo ambapo atakuwa
akihudhuria si kwa cheo chake katika klabu, lakini ifahamike wazi
kwamba Yanga haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe kushiriki
katika shughuli za soka. Tukiwa kama klabu tuko tayari hata kuunga
mkono hatua zozote za kisheria dhidi ya TFF na iwapo TFF itajaribu
kuifungia Yanga, tutalichukua suala hili hadi katika vyombo vya juu
zaidi vya michezo.
2.2. Hata
hivyo, iwapo kuitwa huko kunahusu suala la faini ya Sh. 5 Milioni dhidi
ya Jerry, fedha hiyo ilikwishatolewa kwa TFF.
2.3. Wanaokula
njama ndani ya TFF kuwanyamazisha au kuwafungia ambao wanaeleza mawazo
yao kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, lazima wafahamu kwamba kuikosoa
TFF hakupingani na sheria, na wafahamu pia kwamba Yanga chini ya
uenyekiti wangu haitakubali wanachama au wafanyakazi wa klabu
kudhalilishwa au kutishwa.
3. MKATABA WA TBL NA YANGA
3.1. Mkataba
wa kampuni ya bia nchini (TBL) na YANGA ulisainiwa miaka mitano
iliyopita na mtangulizi wangu. Huu ulikuwa mkataba haramu kwani mamlaka
ya kutia saini mikataba kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yapo kwa
wadhamini na hapana kitu kama azimio kutoka bodi ya wadhamini kuingia
katika makubaliano kama haya, au mkataba kusainiwa na wadhamini.
3.2. Wakati
wa kipindi changu kilichopita, nilijitahidi kurekebisha tofauti zote
zilizokuwepo, lakini nilishindwa. TBL ni mara moja tu imetoa mara moja
tu Sh. 20 Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day zilizoahidiwa
kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu fedha ya marekebisho inayofikia
Sh. 30 Milioni wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka kama
ililoahidi katika mkataba. TBL imejulishwa kuhusu hili lakini
haijalishughulikia.
3.3. Yanga
imeingia katika mkataba wa masoko na kampuni ya International Marketing
ili kupata wafadhili wake, ili kupunguza pengo la TBL kwa ajili ya
mishahara ya Juni. Hii ni kampuni ambayo nilikuwa mwenyekiti wake na
ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo ambalo liliifanya Yanga
kuvaa jezi za nembo yake katika mchezo dhidi ya TP Mazambe.
3.4. Iwapo
wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja katiba kwa maslahi yangu binafsi
au wakiwa na sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo, walifikishe
suala hilo kwenye kamati ya maadili ya klabu kwa ajili ya uamuzi.
4. MUHTASARI
4.1. Nimechaguliwa
katika mazingira ya amani zaidi miongoni mwa vyama vya soka nchini na
ambapo hakuna hata senti moja ilitumika kwa ajili ya kumhonga yeyote.
4.2. Nilisimama
bila kupingwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na nikawaambia wapiga kura
wangu waziwazi kwamba: Wakati huu nikiwa Mwenyekiti sitakaa kimya kwa
wale watakaojikita katika kuhujumu masuala ya fedha klabuni na wale
wanaoamini kwamba TFF iko juu ya sheria zinazohusu masuala ya biashara
na haihusiki na Katiba ya Tanzania. Nawashukuru wapiga kura wangu ambao
walinipigia kura kwa asilimia 100 ya ushindi wangu.
4.3. Masuala
yanayotokea uwanjani au usajili wa wachezaji ni ya soka na kwamba TFF
ina mamlaka ya kuipeleka mbele nchi yetu kwa kufuata miongozo ya
FIFA. Lakini sitavumilia upuuzi wa TFF kutaka kuingilia masuala ya
Yanga. Tunajua FIFA imechafuka kwa rushwa na kusababisha Sepp Blatter
kuong’olewa na kukabiliwa na mashitaka: hata hivyo, iwapo tungetumia
kauli za TFF, Blatter na Platini wasingefanywa chochote.
Masuala
ya fedha ya klabu yetu, yawe kuhusu nembo ya klabu kwenye kituo cha
televisheni bila ya kibali cha Yanga si ya kuamuliwa na TFF. Kilichopo
ni kwamba kitu cha televisheni kinatengeneza fedha kutoka kwa Yanga,
TFF inatengeneza fedha kutoka kituo cha televisheni. Hivyo, iwapo kuna
mtu anafikiri sijui sheria za mashindano bora ya kibiashara na
hakimiliki, basi wajue hilo litawagharimu.
4.4. Iwapo
TFF inataka Mwenyekiti wa Yanga akubaliane na uwongo, basi katika miaka
minne ijayo niko tayari kupambana na uovu huo na kusahihisha kila
kitu. Hata hivyo, kwanza kabisa niko tayari kushirikiana
kirafiki na wakati huohuo kupigania haki za klabu kwani daima nimekuwa
mtu mwenye kupigania haki na masuala ya kikanuni ninayoyaamini ni ya
kiadilifu.
4.5. Yanga
ilikuwepo kabla yangu na itakuwapo baada yangu. Ni wajibu wangu
kuiacha Yanga ikiwa klabu bora zaidi kuliko nilivyoikuta na nikiona
siwezi tena kutumikia maslahi ya wanachama wake, sitasita kujiuzulu au
kuitisha uchaguzi ili kujipanga upya.
5. MWISHO:
5.1. Kwa
mashabiki wa soka wa Yanga na Tanzania nzima, tumefikia hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho si kwa bahati. Mwaka jana tulitolewa kwa
tofauti ya mabao ya kufunga. Na mwaka huu tumekutana na uhasama katika
mechi zetu ambapo tulipigwa mabomu ya machozi, mbali na huko Misri
ambako tulifanyiwa njama mbalimbali. Vilevile TFF nayo imekuwa haitupi
msaada wowote bali kutuhujumu tena. Nasema sitavumilia hujuma hizi
dhidi ya Yanga.
5.2. Sisi
ni klabu ambayo tumejaa ujasiri, hatujalipiza kisasi kwa tulichofanyiwa
wapinzani wetu wakija hapa. Ndiyo, tumeshindwa mechi mbili, lakini kwa
heshima.
Hatutashusha
vichwa vyetu kwa aibu au kutaka kufanikisha mambo yetu kwa njia za
panya. Tutawekeza katika timu yetu kila raslimali.
Natoa wito kwa Yanga kutokata tama katika juhudi za kujenga uwanja wetu juu ya misingi aliyoiacha Mzee Karume.
Tusisahau kwamba tulikuwa msingi wa nguvu zilizomfanya Mwalimu Nyerere kuikomboa Tanzania na nchi nyingi za Afrika.
Historia yetu imejaa kila aina ya fahari.
Tumepigania yote tuliyoyaamini na tumeshinda.
Matumaini
yetu ya kutwaa kombe la ushindi wa ubingwa katika Afrika yako karibu na
kwamba kila hatua tufanyayo inatupeleka karibu na lengo hilo.
Mustakabali
wetu unatuonyesha kwamba kama si mwaka huu, basi mnamo miaka mitatu
ijayo tutafika katika fainali za michuano hii tukishirikiana vyema.
Ni
kweli wasaliti wapo, lakini lazima tusonge mbele, kila tunapokatishwa
na tama na watu wengine, basi tujue tunakaribia ushindi wetu.
5.3. Nataka
kila mtu aamini kwamba hii ni timu yake si yangu mimi. Tunamtaka zaidi
kila mtu hivi sasa kwani tunakaribia katika lengo letu la kutwaa
ubingwa wa Afrika, japokuwa tunafahamu kwamba kuna mengi ya kufanya
lakini mengi zaidi tumeishamaliza, kikubwa matunda yanaonekana na
tunashiriki michuano ya kimataifa tunashiriki na tunapiga hatua moja
mbele.
5.4. Si
rahisi lakini tusilalamike. Hakuna kitu Mungu anatuwekea mbele yetu
bila ya sisi kuwa na nguvu ya kuvuka. Kwa imani, DAIMA MBELE, NYUMA
MWIKO.
Asante.
(YUSUF MEHBUB MANJI)
MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA
Post a Comment