KUHUSIANA NA MSIBA WA MWANDISHI ELIZABETH MAYEMBA...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi
wa Kampuni ya Business Times Limited (BTL), inayozalisha Magazeti ya
Business Times, Majira na Spoti Starehe, unatangaza kifo cha mfanyakazi
wake Elizabeth Mayemba.
Elizabeth
Mayemba ambaye ni Kaimu Mhariri wa Michezo Gazeti la Majira alikutwa na
mauti Jumamosi ya Julai 9, 2016 saa 2 usiku, akiwa nyumbani kwake
Tabata Kisukulu, Dar es Salaam.
Kabla ya kukutwa na mauti, marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote ya kila siku bila kuonesha dalili za kuumwa.
Akiwa nyumbani kwake saa 2 usiku, alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Amana, akiwa njiani alikutwa na mauti.
Kwa
mujibu wa familia ya marehemu, Elizabeth Mayemba atazikwa siku ya
Jumanne ya Julai 12, 2016, mkoani Morogoro kwenye Makaburi ya Kola.
Elizabeth
Mayemba ataagwa Jumatatu ya Julai 11, 2016 saa 5.00 asubuhi nyumbani
kwake Tabata Kisukulu. Baada ya Misa mwili utasifirishwa kwenda Morogoro
kwa mazishi.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kila mara ili kuwapa nafasi watu wengi wajue ratiba zote zilivyopangwa.
Kampuni
imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth Mayemba, ambaye mchango
wake ulikuwa mkubwa zaidi na ulioonekana kwa kila mtu. Marehemu ameacha
mume na watoto watatu wa kiume.
Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Meneja Mkuu
Business Times Limited
Post a Comment