Bella, Wema, Idris Walivyofunika Katika Black Tie
Usiku wa kuamkia leo, staa wa Bongo Muvi,
Wema Abraham Sepetu pamoja na mwandani wake, Idris Sultan waliiongoza
shoo ya Black Tie iliyokuwa maalum kwa King Of The Best Melodies,
Christian Bella iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa King Solomoni, Kinondoni
jijini Dar.
Katika shoo iliyohudhuriwa na mashabiki
kibao, Bella alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 10 tangu aingie kwenye
muziki nchini ambapo aliungwa mkono na mashabiki na mastaa kibao wa
muziki wa Dansi, Bongo Fleva pamoja na Bongo Muvi wakiongozwa na Irene
Uwoya, JB, Steve Nyerere, Shilole, Jacqueline Wolper, Linah, Barnaba,
Faiza Ally, Odama na wengine kibao.
Shoo hiyo iliyoandaliwa na rafiki wa karibu
na Wema aitwaye Muna (Muna Logistic), ilianza mida ya saa nne za usiku
kwa burudani kutoka kwa msanii Nandy na baada ya hapo alifuatiwa Linex
kisha Linah na kumalizia kwa Barnaba ambaye aliwakumbusha mashabiki
Wimbo wa Barua aliouimba zamani na Linah.
Ulipofika muda wa saa nane kasoro, Bella
aliingia jukwaani na kufunika ambapo alipiga nyimbo zake zote kali
kuanzia yapo wapi mapenzi, Nagharamia na nyingine kibao.
Baada ya Bella kufanya shoo ya kwanza,
alimpisha Wema na Idris ambao kwa mara ya kwanza walipanda na
kutambulisha waandaaji wa shoo hiyo.
“Tunawapongeza Muna Logistic lakini pia nimpongeze Bella kwani ndiye msanii pekee aliyeweza kutamba kwa muda mrefu bila kuchuja.
“Bella ameaandaliwa CD, DVD za muziki wake tangu alipoanza na kufikisha hiyo miaka 10,” alisema Wema Sepetu akiitikiwa na Idris.
Kilichofuta baada ya hapo, Walifungua
shampeni spesho (za makaratasi ya kung’ara) ambazo zilipendezesha ukumbi
wote na kulipukwa kwa furaha.
Baada ya kushuka kwa Wema na Idris, MC
mwingine aliyekuwa akiongoza shoo hiyo, Gardner G. Habash aliruhusu shoo
kuendelea kwa Bella ambapo kivutio kikubwa kilikuwa pale alipopanda na
kuanza kuimba Wimbo wa Nani Kama Mama huku akitaja jina la msanii
mmojammoja ambaye ameguswa na wimbo huo kuja kutoa chochote na baada ya
hapo kilichofuatiwa ni mvua ya hela kutoka kwa mastaa kibao wakiongozwa
na Alawi Junior.
Mbali na shoo hiyo, kivutio kingine
kilikuwa ‘red carpet’ ambayo ilikuwa kitofauti na iliyoongozwa na baadhi
ya mastaa wakiwemo Miss Tanzania, Lilian Kamazima.
Imeandaliwa na Andrew Carlos na Musa Mateja/GPL
Post a Comment