HOFU YAREJEA TENA OLD TRAFFORD, MOURINHO AGAWA MAKUNDI MATATU
Wakati
kocha Jose Mourinho akipambana kumnasa Paul Pogba, inaonekana wazi kuwa
kiungo mkongwe Bastian Schweinsteiger ataongoza kundi la ambao
watatemwa.
Tayari
Mourinho amefanikiwa kumsajili mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic
pia Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan ambaye pia ni kiungo, hivyo
nafasi ya Schweinsteiger inakuwa ndogo.
Lakini
kuna wengine walio kwenye hofu ya kutupiliwa mbali ingawa bado kuna
viungo watakuwa na nafasi kama Morgan Schneiderlin, Michael Carrick,
Ander Herrera na Marouane Fellaini.
Wako wenye hofu kama Marcos
Rojo, Juan Mata, Matteo Darmian, Memphis Depay, Adnan Januzaj na Ashley
Young ambao inaonekana wanaweza kubaki lakini hawana uhakika wa
asilimia mia.
Uhakika wataondoka:
Bastian Schweinsteiger
Marcos Rojo
Matteo Darmian
Bado hawana uhakika 50/50:
Juan Mata
Memphis Depay
Adnan Januzaj
Ashley Young
Uhakika wanabaki Old Trafford:
Marcus Rashford
Guillermo Varela
Will Keane
James Wilson
Tyler Blackett

Post a Comment