Vanessa alazimishwa kudendeka ndani ya Ukumbi wa Bilicanas
NJEMBA mmoja ambaye jina lake
halikuweza kufahamika mara moja, juzikati aliwashangaza watu baada ya
kulazimisha kudendeka jukwaani na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,
Vanessa Mdee ‘V-Money’.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta jijini Dar ambapo
msanii huyo alikuwa akitumbuiza huku akipita kwa mashabiki na kutaka
kuwapa mikono.
Katika hali ya kushangaza, Vanessa
alipofika kwa mwanaume huyo alimpelekea mkono akitaka kumshika kidevu,
ndipo njemba huyo alipomshika mwanadada huyo na kumvutia mdomoni mwake.
Hali hiyo ilimfanya Vanessa afurukute
kujichomoa mikononi mwa mwanaume huyo na kuendelea na shoo huku
akimuacha mshikaji akiwa kamtolea macho.

Post a Comment