Ukawa wavaa nguo nyeusi, wabeba mabango ya ujumbe kwa JPM, Dkt. Tulia
WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia
bungeni wakiwa wamevalia nguo nyeusi wote walipohudhuria kikao cha 54
cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kuingia bungeni na
kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe
mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.
Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma mara baada ya kutoka
nje, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia,
amesema hawajatoka wala kulikimbia bunge, na kwamba wapo bungeni na
wanaendelea kufanya kazi za bunge.
“Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tunahasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia
CHANZO: GPL
“Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tunahasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia
CHANZO: GPL

Post a Comment