Penina amwaga chozi kisa kudaiwa kujiingiza
Jennifer Raymond ‘Penina’
MSANII wa Bongo Muvi anayefanya poa, Jennifer Raymond ‘Penina’ hivi karibuni alijikuta akitokwa na machozi baada ya kudaiwa kujiingiza katika biashara ya kujiuza nchini China.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Penina amekuwa na safari za China na Thailand na kwamba mambo yake kwa sasa ni supa.
Baada ya madai hayo, Amani lilimtafuta Penina na alipopatikana alifunguka;
“Jamani! Jamani! Mimi sijui hata wanajiuzaje? Huwa nakwenda kule kibiashara tu. Ndiyo matatizo ya Wabongo, mwanamke akijishughlisha na kupata mafanikio wanasema anajiuza,” alisema Penina huku akilia.
CHANZO: GPL

Post a Comment