MEMPHIS HAJIAMINI KAMA ATABAKI MBELE YA MOURINHO, AANZA KUHAMA ENGLAND MAPEMAAA
Kiungo
Mholanzi Memphis Depay hana uhakika kama ataendelea kubaki katika
kikosi cha Manchester United chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho.
Depay ameanza kuhamisha vita vyake kurudisha kwao nchini Uholanzi akianza na magari yake ya kifahari.
Gari
lake la kifahari aina ya Mercedes G Wagon lenye thamani ya pauni
100,000 pamoja na pikipiki aina ya Scorpion yenye thamani ya pauni
13,500 pia zimepelekwa kwao Uholanzi.
Tayari
kuna taarifa Mholanzi huyo mwenye miaka 22, alianza kusafirisha gari
lake la kifahari zaidi aina ya Rolls Royce Wraith lenye thamani ya pauni
250,000 kulirejesha kwao Uholanzi. Hata hivyo, bado Mourinho hajaanza
usajili.
Post a Comment