TFF yakubali Yanga kuendelea na Uchaguzi chini ya uangalizi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Juni 7, 2016 limefanya kikao cha pamoja na uongozi wa Klabu ya Young Africans.
Kikao
hicho kilifanyika ofisi ya TFF iliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Ilala jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi
kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine; Kaimu
Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Elliud Mvella; Makamu Mwenyekiti wa
Young Africans, Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka
Deusdedit.
Baada ya mazungumzo, Rais wa TFF, Malinzi ametoa maelekezo yafuatayo:-
1. Mchakato wa Uchaguzi wa Young Africans uendelee.
2. Mchakato huo usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya Young Africans chini ya uangalizi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
3. Wale wote waliochukuliwa fomu za uchaguzi wa Young Africans katika ofisi za TFF washirikishwe kwenye mchakato huo.
Mwisho,
Rais wa TFF Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wanachama na
wapenzi wa Young Africans na kuwa na umoja na mshikamano kuelekea
uchaguzi huo muhimu wa kwa mustakabali wa klabu.
Post a Comment