Mama, Baba Wamtenga Wolper kisa Skendo za Wanaume…
Jacqueline Wolper
DAR ES SALAAM: Jacqueline
Wolper, staa wa Bongo Muvi, ametengwa na familia yake akiwemo mama na
baba yake mzazi kutokana na kukabiliwa na skendo za wanaume kila
kukicha.
Akizungumza na gazeti hili hivi
karibuni, staa huyo alisema migogoro yote ambayo inatokea kwenye familia
yake ilianza mara tu baada ya kuachana na mchumba wake ambaye ni raia
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayejulikana kwa jina moja la
Putin.
Jacqueline Wolper na Harmonizer.
Alisema mwanaume huyo ndiye
anayezungumza uongo kwenye familia yake na kumsababishia aonekane ni
mbaya kwa ndugu zake hadi kufikia hatua ya kumtenga.
“Unajua nilipoamua kushtuka na kuachana
na Mkongo kumekuwa kunaibuka vitu vingi sana katika familia yangu kwa
sababu yeye anajifanya ni mwema kwao na kila anachozungumza wanaona kuwa
anasema kitu sahihi lakini kumbe ni mzushi tu, amewajaza maneno kibao
kuhusu mimi na wanaume,” alisema Wolper.
Staa huyo alizidi kufunguka kuwa, baada
ya kuamua kuachana na Mkongo huyo kwa kitendo alichomfanyia hasa cha
kumtelekeza hotelini Afrika Kusini, ameamua kutulia na mpenzi wake wa
sasa ambaye pia ‘anachafuliwa’ na Mkongo.
“Najua kabisa kinachomuuma Mkongo ni
mimi kuwa na mpenzi mwingine lakini nashangaa sana maana yeye alinitumia
ndivyo sivyo sasa matokeo yake nilipochoka na kuamua kuendelea na vitu
vyangu ndiyo anawaambia vitu vya uongo mama yangu na ndugu zangu,
wanatengeneza sumu ya kunichukia mimi,” alisema Wolper.
Akizidi kutema cheche kwenye kinasa sauti cha Risasi Jumamosi,
Wolper alisema alimsihi mpenzi wake huyo wa zamani (Mkongo) kumuacha na
familia yake kwa sababu mapenzi yalishaisha zamani, asimharibie
nyumbani kwao na akumbuke wale ni ndugu zake wa damu, ipo siku watakaa
na kuyamaliza.
“Namshangaa sana kwa kweli, akumbuke
kabisa jitihada anazofanya kuniangusha na hata kuniaibisha zitagonga
mwamba tu kwa kuwa sumu anayoieneza kwenye familia yangu mwisho itakuwa
aibu yake kwa kuwa wale ni damu zangu, nitayamaliza yeye atabaki na
aibu,” alisema Wolper.
Kabla ya kuachana na Mkongo na
kuhamishia majeshi kwa mpenzi wake wa sasa, Wolper alishawahi kutembea
na mfanyabiashara maarufu kwa jina la Dallas ambaye alimwagana naye
baada kushindwana tabia licha ya kuwa alishambadilisha hadi dini Wolper
na kuwa Muislam.

Post a Comment