MALINZI ATUMA PONGEZA ZA USHINDI WA UCHAGUZI KWA MANJI
Baada
ya mzozo mkuuubwa kati ya Yanga na TFF kuhusiana na uchaguzi, hatimaye
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza
Yusuf Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Young Africans SC
baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa. Kura mbili
ziliharibika kwa nafasi hiyo.
Kadhalika
Rais Jamal Malinzi amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428 wakati mpinzani wake Titus
Osoro alipata kura 80. Kura 1,508 zilipigwa katika nafasi ya kuwania
makamu mwenyekiti.
Kadhalika
wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Utendaji kwa kuchaguliwa kuongoza
Klabu ya Young Africans kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa katiba.
Wajumbe
waliochaguliwa ni Omary Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi
(894), Thobius Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay
(818), Hussein Nyika (770) na Hashim Abdallah (727.
Katika
salamu hizo za pongezi, Rais Jamal Malinzi pia amewapongeza wanachama
wa Young Africans kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.
Kutokana
na hali hiyo, Rais Jamal Malinzi amewataka uongozi huo wa Young
Africans kufungua ukurasa mpya wa kuendesha klabu hiyo na kuiletea
mafanikio klabu hiyo kongwe na maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika
Mashariki na Kati hasa wakati huu ambako Young Africans inashiriki hatua
ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Post a Comment