ad

ad

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge-4

 
 MTUNZI: Irene Mwamfupe Ndauka
ILIPOISHIA : “Yaani akinipa dakika tatu tu ya kunisikiliza atajua mimi ni nani na ninaamini ataingia laini,” alisema moyoni Jombi huku macho yake yakitamani sana kumwona anayetoka. SASA ENDELEA NAYO MWENYEWE... MWANAUME mmoja mnene, mrefu, mweusi tii ndiye aliyetoka akiwa amevaa singlendi kwa juu, chini pensi. Alionekana ana asili ya ukorofi... “Mbona umesimama hapo kijana, una shida na nani?” aliuliza yule mwanaume huku akikohoa. “Hapana, napita tu,” Jombi alijibu kwa upole huku akianza kutembea. Lakini muda huohuo, mama Mei alichomoza kwenye mlango mkubwa, akashuka ngazi na kuelekea uelekeo wa ile baa waliyokaa. Kwa usiku ule na kwa kutumia mwanga wa taa ukijumlisha na tembea yake, hata yule mwanaume pale nje alimwangalia kwa macho yenye matamanio makubwa...
“Haya bwana, ulimwengu shujaa,” alisema yule mwanaume huku mama Mei kama vile anafanya kusudi sasa, maana ungeweza kusema mzigo utaanguka wakati wowote ule. Jombi alitamani kugeuza njia kwani aliamini mama Mei anarudi kule baa kwa ajili yake. Alichofanya, alikatiza mbele akageuza kwa njia nyingine na kutokea baa. Alivuta kiti na kukaa huku macho yake yakimulika kila kona kama atamwona mama Mei. Lakini hakumwona! Jombi alijisikia unyonge sana, akaondoka kurudi kwake lakini safari hii akitumia njia nyingine. *** Ilikuwa siku iliyofuata asubuhi, mzee Hewa alikuwa uani akipiga mswaki ili afuate mafao yake, NSSF, mama Mei alitoka ndani kwake akiwa ndani ya kanga moja tu... “Shikamoo mzee Hewa...” “Marahaba mwanangu, umeamkaje mama?” aliitika mzee huyo huku akimwangalia mama Mei anavyokwenda chooni huku wowowo likisomeka kwa baba mwenye nyumba wake
kwa mtetemeko... “Leo mbona asubuhi sana mzee Hewa?” mama Mei alimuuliza bila kusimama... “Nafuata vijisenti vyangu NSSF bwana...” “Ahaa! Kavilite tule hata nyama,” mama Mei alimtania mzee huyo. Mzee Hewa hakuongeza neno kwani tayari mama Mei alishazama chooni åΩLakini wakati anatoka, baba Mei naye alikuwa ameshatoka alikuwa uani hapo akipiga mswaki. Kwa hiyo mzee Hewa alishindwa kutia neno mbele ya mali za watu... “Hivi wewe mbona hunisikii?” baba Mei alimuuliza mkewe kwa sauti ya chini lakini yenye hasira sana, mama Mei hakujibu, akaenda ndani. Kwa mzee Hewa baba Mei kumlalamikia mkewe kwamba hamsikii ilikuwa kama mara ya saba tangu wamehamia pale... “Kama ni mara saba je mara ambazo mimi sijasikia ni ngapi? Kuna jambo, huyu mama hataki kumsikia mume wake na hawa ndiyo wanawake wetu siku hizi,” alisema moyoni mzee huyo, akaenda kuoga akarudi
ndani kwake kujiandaa. Baba Mei ndiye aliyeanza kutoka ndani ya nyumba ile. Wakati mzee Hewa anatoka, alimwita ili ampe lifti... “Ameshaondoka mbona,” alijibu mama Mei... “Ooo! We upo?” mzee Hewa alimuuliza akiwa amesimama mlangoni, mama Mei akatoka huku na kusimama mlangoni... “Mimi nipo baba,” alisema mama Mei. Mzee Hewa alimwangalia mama Mei, mama Mei naye akagundua anamwangalia, wakaangaliana, mama Mei akainamisha uso... “Hivi mjukuu wangu...” “Abee...” “Mumeo anapenda kukulalamikia kwamba humsikii, kuna nini kati yenu?” Mama Mei akaachia tabasamu... “Mzee Hewa, baba Mei hana lingine zaidi ya wivu. Yeye hataki mimi nivae kanga, nivae suruali, anataka nivae magauni makubwa tu...sasa kwa mfano saa zile natoka kwenda chooni, nivae gauni kama nakwenda kanisani, inawezekana kweli..?
“Haya, kama vile haitoshi, hali ya jiji letu la Dar inafahamika, sasa mchana na jua kali mimi naenda sokoni, nivae gauni kama nakwenda kwenye mkutano wa wazazi shuleni, ni sawa kweli?” Mzee Hewa alibaki akisikiliza, ikafika mahali akasema... “Kuna dozi yake nitakupa...” “Ya kunywa ya kumeza?” aliuliza kwa haraka mama Mei... “Ya kawaida tu, wivu wote huo utakwisha...” “Kweli mzee Hewa? Maana ananikwaza sana ujue...” “Dawa yake ndogo tu nitakupa dozi mimi,” alisema mzee huyo huku akiondoka... “Mzee Hewa naisubiri kwa hamu kubwa hiyo dozi,” mama Mei alimsindikiza kwa maneno hayo. *** Alasiri ya saa tisa, mzee Hewa alirudi kabla baba Mei hajarudi, alimkuta mama Mei amekaa nje kwenye mkeka... Je, nini kilitokea hapo?  Usikose kusoma kwenye Ijumaa, Ijumaa

No comments

Powered by Blogger.