Exclusive Wastara mjamzito
Wastara Juma.
Exclusive! Habari mpya ya motomoto ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo,
Wastara Juma amenasa ujauzito, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza
kukupa mchapo huu!
Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe,
Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo
cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka
ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.
Taarifa kutoka kwa vyanzo, zinaeleza
kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa
anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini Risasi
Jumamosi lilichimba na kupata ubuyu ulionyooka kuwa aliondoka nchini kwa
ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.
NDUGU AVUJISHA UBUYU KAMILI
Ndugu wa karibu na Wastara ambaye
hakupenda jina lake lichorwe gazeti, amefunguka kuwa baada ya Wastara
kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda
Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia
alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake?
Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana
anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.
NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa
mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu
aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa
akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni
alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa
hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na
ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Baada ya habari hiyo kutua Risasi Jumamosi, Wastara alitafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, akafunguka:
“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu
wanaongea sana, nimeondoka nchini kwa shughuli zangu binafsi lakini
maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea
kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa
jumla.”
Risasi Jumamosi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au la?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini?
Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua
niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.
TUJIKUMBUSHE
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu
baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo
ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.
Post a Comment