BREAKING NEWS: MANJI, CLEMENT SANGA KUCHUKUA FOMU KESHO
SANGA (KUSHOTO) AKIWA NA MANJI. |
Baada
ya ukimya, sasa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na makamu wake,
Clement Sanga wanachukua fomu za kugombea nafasi hizo, kesho.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema, Manji na Sanga watachukua
fomu za kugombea tena nafasi hizo, kesho saa sita mchana.
“Ni kweli tuna taarifa hizo, maana siku ni moja tu na Manji na Sanga watajitokeza kesho,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Pamoja
na TFF kutangaza uchaguzi "wake" wa Yanga, Uchaguzi wa Yanga chini ya
klabu ya Yanga umepangwa kufanyika Juni 11 na ratiba kamili iko hivi.
Tarehe
1/6/2016. Kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga, nafasi zinazogombewa
na kubandika kwenye mbao za matangazo.Mhusika/ Katibu Mkuu.
Tarehe
2-3/6/2016. Kuanza kuchukua fomu za ugommbea. Mwisho wa kuchukua na
kurudisha fomu za kuomba uongozi. Mhusika/ wagombea wote
Tarehe
4/6/2016. Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za
kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali na kuchapisha na kubandika
kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.
Mhusika/ Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.
Tarehe 5/6/2016. Kipindi cha kupokea na kuweka mapingamizi kwa mgombea. Mhusika/ Kamati ya uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.
Tarehe
6-7/6/2016 Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa awali, kupeleka
majina TFF ilikuhakikiwa, kusikilizwa na kutolea maamuzi ya masuala ya
maadili na kukata rufaa kwa maamuzi yaliotolewa, Kusikilizwa rufaa na
kutoa maamuzi ya rufaa na kisha kutangaza majina ya wagombea. Mhusika /TFF.
Tarehe a7-10/6/2016 Kipindi cha Kampeni kwa wagombea. Mhusika/ Wagombea.
Tarehe 11/6/2016 Uchaguzi wa Yanga. Mhusika/ Wanachama
Tarehe 12/6/2016 Kutangaza matokeo. Mhusika/ Wote.
Post a Comment