YANGA WANATAKA MAKOMBE SI NDIYO? SOMENI HAPA ANACHOKISEMA TAMBWE
Straika
nyota wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, leo atakuwepo uwanjani wakati
timu hiyo ikivaana na Azam FC katika fainali ya Kombe la FA, lakini
kubwa zaidi ameahidi kuipa mataji mbalimbali likiwemo hilo.
Yanga
inatarajiwa kuvaana na Azam katika fainali hiyo ya FA itakayopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mchezo unatarajiwa kujaa
upinzani mkubwa.
Mrundi
huyo, tayari ameiwezesha timu hiyo kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu
Bara, huku akiipeleka Yanga hatua ya makundi ya Nane Bora ya Kombe la
Shirikisho Afrika mwaka huu. Tambwe alitokea Simba iliyositisha mkataba
naye kwenye usajili wa dirisha dogo msimu uliopita.
Tambwe
alisema katika mechi zote atakazocheza, atahakikisha anatimiza majukumu
yake ya kufunga mabao ili aiwezeshe timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali,
ukiwemo ubingwa wa leo.
Tambwe
alisema, hiyo ndiyo kazi yake, kufunga mabao kuhakikisha anaipa
mafanikio timu yake inayofundishwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm na
Juma Mwambusi.
Aliongeza
kuwa, pia ataendelea kufunga mabao ili aendelee kuchukua ufungaji bora
kwenye kila mashindano baada ya kutwaa mara mbili kwenye misimu miwili
tofauti ya ligi kuu msimu wa 2013/2014 na 2015/2016.
“Kati
ya vitu ambavyo vinanipa furaha, basi haya mafanikio ninayoyapata
nikiwa ninaichezea Yanga, kiukweli nafurahi sana kuiwezesha timu yangu
kutwaa taji la pili la ubingwa wa ligi kuu.
“Hivyo
nimepanga kuendelea kuipa mafanikio zaidi timu yangu ya Yanga pamoja na
mimi mwenyewe kupata mafanikio kama haya unayoyaona ya kuchukua
ufungaji bora msimu huu,” alisema Tambwe.
Post a Comment