WACHEZAJI LEICESTER CITY WAULA, MILIONEA AWAZAWADIA MAGARI YA UMEME
Wachezaji wa Leicester City pamoja na bench la ufundi watafaidika kwa kupewa magari aina ya
Mercedes Benz.
Hii
ni baada ya timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England na
kuwashangaza wengi ambao waliamini ingekuwa ni timu ya kupambana kuepuka
kuteremka daraja.
Mmiliki
wa timu timu hiyo aria wa Thailand, Vichai Srivaddhanaprabha ameamua
kutoa magari 30 aina ya Mercedes B-Class Electric Drive ambayo yanatumia
umeme badala ya mafuta ili kuendesha injini yake.
Magari hayo ya kisasa yatakabidhiwa kwa wachezaji na watu wa bench la ufundi.
Bei ya gari moja aina ya Mercedes B-Class Electric Drive ni pauni 32,670 (zaidi ya Sh million 103).
Kabla
ya hapo, milionea Srivaddhanaprabha alishawaahidi wachezaji na benchi
la ufundi la Leicester safari ya kwenda kula bata jijini Las Vegas,
Marekani.


Post a Comment