Viashiria 11 kuwa mpenzi wako anakuhitaji faragha!
BILA
shaka mpenzi msomaji umzima bukheri wa afya, huna budi kumshukuru
Maulana kwa kukufikisha hapo ulipo na leo umeweza kukutana nami kwenye
kujadili mada hii kuhusu viashiria 11 kuwa mpenzi wako wa kike
anakuhitaji faragha.
Kiuhalisia wanawake wengi wameumbwa na
hulka ya aibu, kiasi kwamba ni ngumu sana kusema moja kwa moja pale
anapohitaji kukutana nawe faragha. Hivyo sehemu kubwa ya sema yao
huwakilishwa na vitendo;
Macho
Macho ya mwanamke yanazungumza sana kwa
kitu anachohitaji, ukijaribu kuyachunguza vizuri macho yake kuna kitu
utakiona kinaashiria katika mboni za macho ya mpenzi wako, kama vile
yanasinzia au yanakuwa kama amekula kitu kinachomfanya apatwe na
kiusingizi cha mbali. Hii ni moja ya dalili.
Nimekumiss sana mpenzi wangu
Anaweza asiseme moja kwa moja lakini
neno nimekumisi kwake likawa ni zaidi ya kumbukumbu kama ambavyo wengi
wamelizoea, kumbe yeye akawa anamanisha amekumisi kwa maana ya
kukuhitaji.
Mazungumzo
Ukijaribu kusikiliza sehemu kubwa ya
mazungumzo yake ni kama huyaelewi vile, mara kasema hiki mara kile, hizo
ni dalili kuwa anahitaji haki yake ila hawezi kusema.
Uchokozi wa hapa na pale
Wakati mwingine anaweza kuanzisha
uchokozi ambao kimsingi anafahamu atakukera au kukukwaza pamoja na
kumkataza bado akaendelea tu kufanya huku anacheka tena kicheko kama cha
kejeli vile, shtuka weweee!
Hatulii
Kama mko ndani unaweza kumuona mwenzako
hatulii, mara nyingi anakuwa anachezea viganja vyake kwa kuvisungua au
kuchezea kucha zake.
Stori za kukufurahisha
Unaweza kushangaa mbona leo kachangamka
sana au kafurahi kupita siku nyingine na pengine siku hiyo anapiga stori
za kutosha na kufurahisha mpaka unamshangaa.
Kukusikiliza kwa upole
Unaweza ukaongea sana lakini muda wote
akawa makini kukusikiliza kwa kila unachokizungumza kiasi cha kushangaa
na tena anakuwa ni mpole kupindukia.
Maongezi yenye bashasha
Wakati mwingine hata maongezi yake
yanakuwa yamejaa bashasha, hana haraka na wewe wala hata hakumbuki kama
kuna kazi nyingine anapaswa kufanya.
Ukimgusa hachukii
Kama ikitokea ukapeleka mkono wako
kwenye moja ya kiungo chake basi hatajisumbua kukutoa bali anaweza
kujifanya kama vile hujamgusa.
Sitaki, nataka!
Mnaweza mkakubaliana kitu lakini ndani
ya dakika mbili akageuka na kusema jambo lingine ila kukaa kwake anakuwa
hajamaanisha bali ni mbwembwe tu za kike.
Aina ya uvaaji
Nguo nazo zinaweza kumsemea mpenzi wako
kile anachohitaji. Kwa mfano kaenda kuoga kisha kaja na nguo nyepesiii
au anaweza kujifanya kakaa vibaya bila kukusudia,ukiona hivyo ujue kuna
kitu anahitaji kwako!
Ni hayo tu kwa leo ni imani yangu kwamba
utakuwa umepata elimu ya kukusaidia kumsoma mpenzi wako kupitia matendo
yake anapokuhitaji.
Post a Comment