Majina ya wahitimu kidato cha sita 2016 wanaotakiwa kujiunga na JKT
Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari
kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara
kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda
kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti
makambini kuanzia tarehe 01 – 05 Juni 2016.
Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma –
Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma,
JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba –
Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical
disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi
mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za
michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia
baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora,
JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze
kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa,
uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na
kulitumikia Taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 20 Mei 2016
Post a Comment