URAIS WA CONGO WAMPONZA KATUMBI, JESHI LA DR CONGO LAMZIGIRA KWAKE, TAARIFA ZAELEZA NI FIGISU ZA RAIS KABILA
Takribani
saa 14 tu baada ya mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe
kutangaza nia yake ya kuwania Urais wa DR Congo, askari wa jeshi la nchi
hiyo wameizunguka nyumba yake anayoishi.
TP
Mazembe ndiyo timu aliyochezea Mtanzania, Mbwana Samatta na kupata jina
kubwa kabla ya kujiunga na KRC Genk ya Ubeligiji. Lakini bado
Mtanzania, Thomas Ulimwengu anaendelea kuichezea timu hiyo.
Taarifa
zimeeleza, Serikali ya DR Congo imetoa kigali cha kukamatwa kwa Katumbi
kwa maelezo kwamba amekuwa akikiuka mambo kadhaa na tayari wizara ya
ulinzi ya DR Congo imesema inataka afunguliwe mashitaka.
Hata
hivyo kumekuwa na taarifa za kutaka kumbana Katumbi ikielezwa Rais
Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambacho ni kirefu cha
DR Congo anaonekana kutofurahishwa na hilo.
Katumbi ambaye anaaminika kwa sasa ndiye Mkongo maarufu kuliko wote duniani, amekuwa presha kubwa kwa Rais Kabila.
Bado
haijaelezwa mwisho wa askari hao wa DR Congo, lakini taarifa nyingine
zimesema Katumbi analindwa na askari kutoka Marekani na Afrika Kusini
ambao wana mafunzo ya juu kabisa.


Post a Comment