Lulu awapa makavu mastaa wapenda kiki
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi wanapenda kiki kuliko kusaka
fedha kitu ambacho yeye hakifanyi.
Akizungumza na gazeti hili, pasipo
kuwataja majina, Lulu alisema anashangazwa na tabia ya mastaa wengi kuwa
‘bize’ kutafuta kiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii badala ya
kukutana pamoja na kufikiria ni kitu gani wanaweza kufanya ili waendelee
kimaisha.
“Jamani mimi nashangaa siku hizi huku
mjini mastaa wanatafuta kiki sana kuliko kufikiria mbinu ya kusaka hela
yaani ni shida kabisa, tubadilike jamani, muda unakwenda,” alisema Lulu.

Post a Comment