Wolper: Lazima nimzalie Harmonize
MTOTO wa Kichaga anayetikisa anga la
Bongo Muvi, Jacqueline Wolper amenyanyua kinywa chake na kusema; “lazima
nimzalie Harmonize (Rajabu Abdulhan, staa wa Bongo Fleva), kwa kuwa
nimeridhika naye.”
Kauli hiyo imekuja zikiwa ni siku chache
tangu mwigizaji huyo aamue kuanika uhusiano wake hadharani kupitia
mitandao ya kijamii ambapo watu wengi wamekuwa wakimsema vibaya kwamba
hayupo ‘serious’ na penzi hilo. Alipoulizwa na mwanahabari wetu kuhusu
madongo hayo, alifunguka:
“Hawajui mimi ndiyo nimefika. Kudhihirisha hilo labda niwaambie tu, nampenda kufa na ni lazima nimzalie Harmonize.”

Post a Comment