KUMBUKA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA MSIMU HUU NI MADRID DERBY

Real Madrid imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 katika jiji la Milan nchini Italia.
Madrid
imetinga fainali hiyo ikiwa ni ya 17 kwake na imefanikiwa kutwaa
ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 10 ambayo ni mara nyingi zaidi
kuwahi kuchukuliwa na timu yoyote ya Ulaya.
Wakati Madrid inatinga fainali hiyo leo, jana wapinzani wake wakubwa na hasimu namba moja kwao Atletico Madrid, walitinga fainali wakiing'oa Bayern Munich inayofundishwa na Pep Guardiola.
Licha
ya ushindi wa mabao 2-1, lakini Bayern imeshindwa kuwazuia Atletico
Madrid ambao wamefuzu kwa bao la ugenini lililofungwa na Antoine
Griezmann.
Sasa
ni derby ya Madrid nchini Hispania inakwenda kuchezwa katika ardhi ya
Italia huku kukiwa na kumbukumbu ya miaka michache tu kuhusiana na derby
of Madrid kuchezwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mwaka
2014, Madrid ilibeba ubingwa wa Ulaya kwa kuifunga Atletico Madrid
katika fainali, mechi ilichezwa Lisbon, Ureno. Atletico imerejea fainali
ikiwa na kocha wake yuleyule, yaani Diego Simeone lakini Madrid
imetinga fainali ikiwa na Zinadine Zidane. Wakati ule ilikuwa chini ya
Carlo Ancelotti.
Mwaka
huo, Madrid ilitinga fainali kwa kuing'oa Bayern Munich na Atletico
ikaiondoa Chelsea. Mwisho Madrid wakawa mabingwa baada ya kupata bao
dakika za mwisho lililolazimisha mpira kwenda dakika 30 zaidi. Mwisho
Madrid ikafanikiwa kushinda kwa mabao 4-1.
Katika
nusu fainali, timu mbili za hispania ziliingia ambazo ni Madrid na
Atletico huku England ikiingiza timu moja, Manchester City na Bayern
Munich kutoka Ujerumani. Mwisho timu zilizotinga fainali zote ni kutoka
Hispania.
Hii inaonyesha muendelezo wa timu kutoka Hispania kuendelea kufanya vizuri katika michuano mikubwa ya Ulaya.
Post a Comment