Kesi ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ mpaka 2017

Kesi ya staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ya kudaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba huenda ikaanza kusikilizwa mwakani (2017), Amani limeambiwa.

“Wale ambao walikuwa na shauku ya kujua kitakachojiri, hayo mambo ni mwakani maana mpaka sasa kesi ambazo zinapewa kipaumbele ni za watuhumiwa ambao wapo mahabusu magerezani. “Ujue kuna kesi nyingi ambazo hazijasikilizwa.
Kwa hiyo hizo ndo’ zinapewa nafasi ya kwanza kuliko kesi kama ya Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana,” kilisema chanzo hicho. Ili kujiridhisha, gazeti hili lilimtafuta wakili wa msanii huyo, Peter Kibatala ambaye alijibu kwa kifupi: “Binafsi sifahamu kuhusiana na hilo, mpaka sasa sijajua hiyo kesi itakuwa lini kwa sababu sijaona ikipangiwa siku.”
Post a Comment