Jokate na siri ya mwanaume anayemtesa

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
Stori: Boniphace Ngumije
DIVA anayefanya vizuri kwenye
tasnia ya urembo na mitindo Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa
‘drama’ zinazoendelea kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi nyingi hazina
ukweli na ukweli anao moyoni.
Akipiga stori ‘direct’ na gazeti hili
hivi karibuni, Jokate alikiri kuwa ana mpenzi ambaye anampenda sana
lakini kwa bahati mbaya mpenzi huyohuyo anamuumiza sana lakini akakataa
kumtaja jina alipobanwa na mwanahabari wetu.
“Kiukweli mtu niliyenaye ni sahihi
kwangu, ninampenda sana japo na yeye kuna namna fulani ananitesa lakini
kiukweli kwake nimefika na Mungu akipenda si muda mrefu watu
watamfahamu,” alisema Jokate.
Hata hivyo, miezi ya hivi karibuni
Jokate alikuwa akibanjuka kimalovee na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ ambaye
inasemekana wameshamwagana.
Post a Comment