Nay wa Mitego Avunjiwa Kioo Cha Gari yake..Alikuwa Anaenda Kutambulisha Video ya Shika Adabu yako
Rapper Nay
wa Mitego amekutwa na misukosuko ya kuvunjiwa kioo cha gari lake na
watu wasiofahamika wakati anaenda kutambulisha video yake mpya ya shika
adabu yako kwenye kipindi cha FNL cha EATV.
Kupitia
akaunti yake ya instagram @NayTrueboy rapper huyo ameweka picha ya gari
hiyo ikiwa imevunja kioo na kuandika maneno yafuatayo..
”Nimevunjiwa kio Cha gari nikiwa njia naenda kwenye Intrvw Chanel5 EaTv kwa ajili ya kutambulisha my New Video #ShikaAdabuYako sorry Watu wangu mliokua mkisubiri kuona Video Na Interview yote nimeshindwa kufika naweka sawa ili. Video itaenda YouTube kesho itakua kwenye Tv yako Pendwa. Muziki sio vita….. I will never stop doing what i do.!!“

Post a Comment