ad

ad

Moyes: Van Gaal apewe muda zaidi Man Utd

Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes amesema klabu hiyo haifai kumfuta kazi Louis van Gaal licha ya klabu hiyo kuandikisha matokeo mabaya.

Kumekuwa na ripoti kwamba klabu hiyo imejiandaa kumfuta meneja huyo na kumpa kazi Mreno aliyefutwa kazi Chelsea mwezi Desemba Jose Mourinho.

Moyes, aliyefutwa kazi na klabu hiyo baada ya kufanya kazi miezi kumi pekee, amesema klabu hiyo haifai kupata sifa za “klabu inayofuta mameneja kiholela”.

Amesema ingawa klabu hiyo ilishindwa na klabu ya Midttyland FC ya Denmark katika mechi ya Europa Leauge Alhamisi, bado kuna mechi ya marudiano nyumbani ambayo wanaweza kushinda.

Moyes mesema alisikitika sana alipofutwa kazi baada ya kufanya kazi miezi kumi pekee.

No comments

Powered by Blogger.