ad

ad

BABA MZAZI WA ISHA MASHAUZI KUZIKWA LEO SAA 6 MCHANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mzee Ramadhan Makongo (pichani kushoto) – baba mzazi wa mwimbaji Isha Mashauzi aliyefariki Jumamosi alfajiri, anazikwa leo Jumatatu Februari 15, saa 6 mchana jijini Dar es Salaam. Baba yake Isha Mashauzi atazikwa kwenye makaburi ya Msingwa, Mbezi kwa Msuguri.


 Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Msuguri ambapo vitu vyote vitafanyika hapo ikiweo kisomo, sadaka ya chakula pamoja na kumswalia marehemu kabla ya kwenda kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele.

 Mtoto wa marehemu, Juma Ramadhan ameiambia Saluti5 kuwa hiyo ndio taarifa rasmi na sahihi baada ya kuwepo vuguvugu la sintofahamu juu ya wapi baba yake azikwe kati ya Dar es Salaam na Musoma.

 Ramadhan Makongo ambaye pia ni baba wa mwimbaji wa taarab Saida Ramadhan na mume wa mwimbaji Rukia Juma, alifariki katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

No comments

Powered by Blogger.