Makonda aongoza upimaji magonjwa ya moyo Dar

Makonda
akihojiwa na wanahabari leo wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa ya
moyo uliofanyika bure na madaktari kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), katika viwanja vya Leaders Club Dar.

Mkuu
wa Kitengo cha Moyo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Peter Kisenge
(kushoto) akizungumza na wananchi kabla ya zoezi la upimaji kuanza.

Umati wa wananchi waliojitokeza kupima afya zao.

Huduma zikianza kutolewa kutoka kwa madaktari hao.

Hapa ni sehemu ya kupata msaada wa huduma mbalimbali.

Makonda (kulia) akishuhudia namna wagonjwa wanavyopatiwa majibu baada ya kumaliza kupatiwa matibabu.

Madaktari wakimsaidia mgonjwa aliyezidiwa ili kupelekwa Hospitali ya Muhimbili.

Mgonjwa huyo akiingizwa kwenye gari maalum kupelekwa Muhimbili.
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Mkaonda, leo ameongoza wananchi wa wilaya
yake na wakazi wengine wa jiji la Dar es Salaam katika upimaji wa
magonjwa ya moyo uliofanyika bure na madaktari kutoka Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI), katika viwanja vya Leaders Club Dar.
Akizungumza
na wanahabari, Makonda kwenye zoezi hilo amesema kuwa wananchi
waliojitokeza wataweza kupata fursa ya kubaini magonjwa mbalimbali kwani
wengi hawajui magonjwa ya moyo jinsi yanavyoweza kusababishwa na
shinikizo la damu ikiwa ni chanzo cha magonjwa ya macho kiharusi, figo
na hata kutokuzaa.
Amesema ugonjwa wa moyo ni hatari na asilimia kubwa ya wagonjwa hao wanatembea na kufanya kazi zao kwa kuwa ugonjwa huo hauna dalili ya haraka na hivyo ni vyema kila mmoja kupima na kujua afya yake.
Amesema wagonjwa watakaokutwa na magonjwa yanayoshabihiana na moyo watapatiwa tiba katika hospitali za jiji la Dar ikiwemo Hospitali ya Kinondoni ya Mwananyamala, na wale watakaokutwa wamethirika zaidi na ugonjwa huo watapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Aidha aliwataka wananchi kuelewa matibabu yake ni gharama kubwa hasa kwa wale wanaosafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Zoezi hilo ni la siku moja lakini kutokana idadi ya wananchi waliojitokeza kuwa wengi zoezi hilo linaweza kuendelea hadi kesho mpaka idadi ya namba za wanaohitaji huduma zitakapomalizika.

HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment