Wawili wafariki, 36 wajeruhiwa katika ajali Morogoro
Basi la BM lenye namba za usajili
T619 BOX baada ya kugongana na lori leo eneo la Lubungo Mikese,
barabara ya Morogoro-Dar es Salaam.
WATU wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne
vibaya baà da ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es
Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori
lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya
barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara
kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
Muonekano wa nyuma wa basi hilo.
ITV imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kushudia
majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM wakiletwa kwa magari binafsi na
basi jingine la kampuni hiyo, wakionekana kujeruhiwa zaidi maeneo ya
kichwani, usoni na miguuni, ambapo mwandishi alilazimika kuweka kalamu
pembeni na kusaidiana na wananchi wengine kuwabeba majeruhi na
kuwaingiza kwa madaktari kupata huduma ya kwanza,huku vitanda vya
kuwabebea vikionekana kuwa vichache ikilinganishwa na wingi wa
majeruhi. Baadhi ya mashuhuda waliohojiwa wameeleza namna ajali hiyo
ilivyotokea na kulalamikia wizi uliofanywa na waliofika eneo la tukio
baada ya ajali.Daktari bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Francis Semwene, amekiri kupokea miili ya wanaume wawili na majeruhi 36, ambapo wanne kati yao hali zao ni mbaya na wengine italazimika kuwakata baadhi ya viungo iwapo watashindikana kushonwa.

Post a Comment