ad

ad

Majungu yenu yatamtoa Kerr Simba


HAKUNA kitu kingine zaidi ya majungu. Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema anaipenda sana timu yake ila kuna kitu kimoja kinaweza kumtoa katika kikosi hicho, nacho ni majungu.

Kerr anayepambana kuhakikisha Simba inarudi katika makali yake, alisema pamoja na jitihada zake zote anazofanya, anachoka kwani majungu na maneno maneno ya baadhi ya watu wasiopenda mafanikio yake vimezidi.
 

Alisema tangu alipojiunga na Simba, amekumbana na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ile ya kuzushiwa mambo ya ajabu ambayo yanamfanya atumie muda mwingi kuyafikiria kuliko kazi yake.
 

“Kitakachoniondoa Simba si kitu kingine bali ni majungu ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakinipiga vita ili nisifanikiwe.
 

“Wananizushia mambo mengi kuwa sijui kufundisha ndiyo maana timu haifanyi vizuri, lakini wote huo ni uongo, ukiangalia mimi na makocha waliopita takwimu zinanibeba lakini chuki tu ndiyo zimewazidi.
 

“Hata hivyo nitaendelea kuitumikia timu yangu mpaka dakika ya mwisho kwa sababu siyo wote wanaonichukia lakini mambo yakizidi, basi nitaondoka ila kwa sasa napambana kwanza,” alisema Kerr.

No comments

Powered by Blogger.