ad

ad

Tambwe: We Maguri! Mimi nina roho mbaya


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, katika kuonyesha amepania kuhakikisha anaibuka na tuzo ya ufungaji bora msimu huu, amempa onyo straika wa Stand United, Elias Maguri kwa kusema yeye ni mchezaji mwenye roho mbaya na hapendi mwingine awe juu yake.
Hadi sasa Tambwe ana mabao 10, akiwa amemzidi bao moja Maguri ambaye ana mabao tisa huku Hamisi Kiiza wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga wakiwa na mabao nane kila mmoja.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe amefunguka kuwa, yeye ana roho mbaya ya kutaka kukaa juu na hataki mtu mwingine ampite.
“Siku zote huwa nina roho mbaya ya kutaka kuwa juu ya wengine, sipendi kuwa chini ya watu wengine hiyo ndiyo sababu kubwa inayonifanya nijitume na kuhakikisha  nakuwa bora kila kukicha.
“Lengo langu ni kuona  nafanikiwa  kumaliza ligi nikiwa mfungaji bora, hivyo najituma kwa nguvu zote, tunahitaji kushinda katika kila mchezo ili kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa mwisho wa ligi,” alisema Tambwe.
 Kiongera agoma Simba
Na Hans Mloli
BAADA ya kiungo wa Simba, Mzimbabwe, Justice Majabvi, kukinukisha kuhusu suala la makazi ya kudumu na yenye hadhi yake, sasa mambo yameanza kunyooka baada ya baadhi ya nyota wa kigeni klabuni hapo kukabidhiwa mijengo lakini Mkenya Paul Kiongera amegoma.
Zoezi la kuwakabidhi nyumba baadhi ya wachezaji hao lilifanyika mapema Jumapili iliyopita baada ya timu hiyo kurejea Dar es Salaam, ikitokea Shinyanga ilikokwenda kuumana na Mwadui FC.
Hata hivyo, nyumba hizo zote zilipatikana maeneo ya Sinza ambapo Mganda, Brian Majwega, Muivory Coast, Vincent Agban na Joseph Kimwaga walikabidhiwa nyumba moja lakini Mrundi, Emiry Nimubona naye akapewa ya kwake kwa lengo maalum la kuishi na familia yake kutoka Burundi kutokana na machafuko ambayo yapo nchini humo.
Tatizo likaja kwa Mkenya, Paul Kiongera, ambaye aligoma kuanza maisha mapya ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi Waganda, Hamis Kiiza na Juuko Murshid, hivyo akalazimika kurejea Rombo Hotel akisubiri suala lake lishughulikiwe ambalo lilitarajiwa kumalizika jana Jumanne au mapema leo.
“Hajaweka wazi sana kwa nini amekataa (Kiongera) kuishi hapo, lakini halikuwa tatizo sana, suala lake linashughulikiwa na mpaka kesho (leo), linaweza kumalizika, ikishindikana basi itakuwa Jumatano mapema sana ili tuendelee na mambo mengine yanayotuzunguka.
“Lakini ukweli ni kwamba aligoma kukaa kwenye nyumba hiyo tena akionyesha kukasirika, kila mmoja alishangaa lakini tunaamini litakwisha,” alisema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.
Powered by Blogger.