Shamsa Ford: Najirusha na mpenzi wangu kokote
MREMBO anayefanya vizuri kwenye anga la filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibua mpya baada ya kudai kuwa akiwa na mtu wake, haoni hatari kujirusha naye mahali popote bila kujali ni wakati gani ilimradi tu eneo la tukio liwe salama na sahihi.
Akichonga hivi karibuni, msanii huyo alisema wakati mwingine yeye na mwandani wake hujikuta katika wakati mgumu kufurahia penzi lao kutokana na kero za Tanesco kukata umeme kiasi cha kuwafanya waamue kwenda hotelini.
“Unajua umeme ukiwa hamna, unakuta nyumbani hakuna mzuka kabisa kutokana na joto la jiji, katika hali kama hiyo mara nyingi mimi na mume wangu mtarajiwa tunakwenda kwenye hoteli yoyote ya karibu kufurahia penzi letu,” alisema.
Post a Comment