Serikali Yapiga Marufuku Matangazo Yote Yanayohusu Tiba asili na Tiba Mbadala Kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii
Taarifa kutoka Wizara ya Afya kuanzia tarehe 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Wale wote wenye vibali
wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba
Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
Utoaji wa elimu ya
afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala
kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi
hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.
Watoa huduma za tiba
asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza
nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia jana Desemba 2015.
Baadhi
ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala,
nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi
katika tiba asili na tiba mbadala
Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia jana 24 Desemba
2015, lipitie nyaraka zote zinazohusu usajili wa watoa
huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za
asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika
huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za
tiba asili na tiba mbadala.
Taarifa hii imetolewa na Dismas
Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John, Kaimu
Katibu Mkuu.
Post a Comment