ad

ad

Nay wa Mitego azinguana na demu wake


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’

BRIGHTON MASALU
KUFUATIA kunaswa na mrembo mpya na picha hizo kuanikwa na gazeti la Risasi juzikati, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ yuko kwenye mgogoro mzito na mpenzi wake aishie Marekani, Stella Tilya ‘Chagga Baby’.


Stella Tilya ‘Chagga Baby’.

Akizungumza na Amani, Nay alisema msuguano uliopo kati yake na mwanamke huyo ni mkubwa kwani picha hizo akiwa na msichana aliyejulikana kwa jina moja la Anna, ambaye alidai kuwa ni rafiki yake wa karibu, umekuwa ni msamiati mkubwa kwa mrembo huyo wa kichaga akidai ameibiwa mali yake.

Mbali na ugomvi wake na mpenzi wake, Nay alisema kuwa hata msichana aliyekuwa naye katika picha hizo (Anna), amefukuzwa nyumbani kwao kwa madai kuwa ameidhalilisha familia yao.

“Dah! Yaani mambo yamekaa vibaya sana, Stella hataki kabisa kunielewa, amekatisha mawasiliano na mimi, nitajitahidi kulimaliza hili,” alisema Nay.
Powered by Blogger.