LOUIS VAN GAAL KAAMUA KUFUNGUKA JUU YA VIPIGO
Baada ya kutoshinda katika michezo mitano mfululizo huku wakipoteza mara mbili mfululizo hadi jana kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ametaka utulivu na mshikamano katika kipindi hiki cha mpito huku akitaka kushinda michezo mitatu mfululizo katika kujiweka nafasi nzuri ya kuwania ubingwa hadi ifikapo Christmas.
Manchester United itacheza na Norwich City kwenye uwanjwa wa Old Trafford kabla ya kusafiri hadi Britannia watakapoikabiri Stoke City na kisha Chelsea ya Mourinho huku kocha huyo muholanzi akisisitiza Manchester United inatakiwa kucheza ligi kwa ajili ya kushinda mataji na kwamba watapambana hadi mwisho.
Akiongea kwa masikitiko makubwa mara baada ya kupoteza mchezo kwa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth kocha huyo amesema matokeo hayo hayakubaliki na kwamba lazima washikamane kuhakikisha wanapata matokeo haraka ili kurudisha imani kwa mashabiki wao.
Aidha Van Gaal amesema kitu pekee kinachotia moyo ni kuona wachezaji wake wakiwa katika morali nzuri na kwamba anaamini wako nyuma yake wanamsapoti na watafanya kazi kwa mshikamano katika kuhakikisha United inapata matokeo.
Wakati huo huo shabiki mmoja wa klabu hiyo akihojiwa mara baada ya mchezo huo wa jana amemtetea Van Gaal na kusema kwamba bado wako katika mbio za ubingwa kwakua wako nafasi ya nne ya msimamo wa ligi wakiachwa kwa tofauti ya points tatu tu kutoka kwa vinara Manchester City.

Post a Comment