Jeshi la Polisi: Vyeti feki vyawaondoa askari kazini ni uzushi
TAARIFA YA
JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na
uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na
kueneza taarifa hizo katika mitandao ya
kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.
Miongoni
mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana
katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa
askari kazini’ Taarifa hiyo ni
uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.
Kufutia
hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la
Polisi kwa jamii.
Jeshi
la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza
taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa
watu wote kuacha kutumia mitandao ya
kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na
badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Imetolewa na:
Advera John
Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu
ya Polisi.

Post a Comment