Ijumaa Sexiest Girl 2015… Nani mshindi kesho? .... Hapa Vee Money, pale Lulu na kule Kidoa!
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mdee ‘Vee Money’
HATIMAYE lile shindano la mwanamke mwenye mvuto (The Ijumaa Sexiest Girl 2015) linatarajiwa kufika kileleni kesho katika Sikukuu ya Krismasi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, unavyodhani nani ataibuka mshindi kati ya Vanessa Mdee ‘Vee Money’ Asha Salum ‘Kidoa’ au Elizabeth Michael ‘Lulu’?
Jibu rahisi, unachotakiwa ni kuhudhuria katika shoo ya Diamond Platnumz itakayofanyika Sikukuu ya Krismasi (kesho) ndani ya Dar Live na kushuhudia mshindi akitangazwa.
Asha Salum ‘Kidoa’
Akizungumza na Amani, mratibu wa shindano hilo, Amran Kaima alisema kuwa usiku huo mshindi atakabidhiwa pesa, tuzo, cheti, ofa ya kufanya shopping ya nguo na kutengenezwa nywele kwa kipindi cha miezi sita.
Post a Comment