ad

ad

Diamond Platnumz afunika Dar Live X-Mass...Picha zaidi ya 20 zipo hapa HISTORIA imeandikwa!




















HISTORIA imeandikwa! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amevunja rekodi ya aina yake kwa kuangusha shoo baab’kubwa usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Ratiba rasmi ya burudani ndani ya ukumbi huo ilianza jana asubuhi kwa michezo mbalimbali ya watoto, msanii wa nyimbo za uswahilini, Msaga Sumu, Wakali Dancers kisha Diamond akamaliza mchezo mzima. Mapaparazi wetu waliokuwepo ukumbini humo; Chande Abdallah, Deogratius Mongella, Denis Mtima, Mayasa Mariwata, Andrew Carlos na Musa Mateja waliripoti shoo hiyo moja kwa moja kwa bosi wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, BamagaMwenge; wasikie mwenyewe: Saa 4:00 asubuhi

MICHEZO YA WATOTO YATAWALA Makao Makuu: Denis najua umefi ka tangu asubuhi hapo ukumbini tuambie nini kimejiri hadi sasa. Denis: Mkuu hapa tayari kumependeza, watoto wanazidi kumiminika wakiwa na wazazi wao. Wanacheza michezo mbalimbali kwenye mabembea, kuogelea na katika ndege maalum iliyopo ukumbini humu. Makao Makuu: Piga kazi nitakurudia tena jioni. Saa 10: 00 jioni

DIAMOND ‘AWASAPRAIZI’ WATOTO
Makao Makuu: Bila shaka Denis utakuwa na kitu, hebu tujuze. Denis: Mkuu hapa watoto walikuwa bize na michezo yao lakini ghafl a, Diamond akaibuka. Watoto wamepagawa. Wanamfuata anasindikizwa na mabaunsa.
Makao Makuu: Duh! Diamond kafata nini tena muda huu shoo si ni jioni? Denis: Eee Mkuu lakini nasikia kaja kufanya ‘sound check’, sasa hapa ni nderemo na vifi jo kwa watoto. Saa 11:00 jioni

DOGO AIMBA WIMBO WA DIAMOND
Deogratius: Mkuu nakutafuta sana hupokei simu, nilikuwa nataka... Makao Makuu: Unanitafuta kwani nimepotea, umenipata sasa leta maneno. Deogratius: Mkuu ni hivi, kuna dogo mmoja kaomba kupanda jukwaani aimbe wimbo wa Diamond huu mpya wa Utanipenda. Sasa hapa Diamond mwenyewe kapagawa jinsi dogo alivyoonesha utundu wa kuimba na kucheza,  huwezi amini Diamond kampa shilingi elfu hamsini papo kwa papo. Makao Makuu: Madogo kama hao ndio wanatakiwa kuendelezwa, enhe nini kinaendelea tena baada ya tukio hilo? Deogratius: Mkuu Diamond kavaa hizi ‘microphone’ za kisasa, anaanza kukagua jukwaa tayari kufanya maangamizi usiku wa leo. Makao Makuu: Safi , huyo ni msanii wa Kimataifa, anajua wajibu wake. Deogratius: Kila kitu kimekamalika, naona Diamond sasa anakwenda kubadili mavazi akisindikizwa na mabaunsa ili arudi kuja kufanya ‘vurugu’ zake. Saa 4:30 usiku

WAKALI DANCERS WAFUNGUA SHOO
Makao Makuu: Enhe Andrew tuambie nini umekiona hapo mpaka sasa, umekuwa kimya muda mrefu. Andrew: Mkuu sasa hivi ndiyo shoo inafunguliwa rasmi. Wakali Dancers, wakali wa ‘kusheki’ ndiyo wameanza baada ya undergrounds kumaliza kufanya yao jukwaani. Saa 5:00 usiku

MSAGA SUMU AJIANDAA
Mayasa: Hapa namuona Msaga Sumu anajiandaa kupanda jukwaani
Mkuu. Anaonekana amepania kweli kukinukisha. Makao Makuu: Namjua huyo ana ngoma zake kama Na Huyu Mtoto, Shemeji Unanitega akiimba hizo itakuwa balaa. Mayasa: Mkuu umetisha sana mi’nilijua unajua kuchapa hadithi tu kumbe hata nyimbo za Msaga Sumu unazijua! Mkuu ngoja nisogee kule nyuma getini naona kuna shangwe nahisi Diamond atakuwa anaingia ukumbini. Saa 5:30 usiku

STARIC ALITAWALA JUKWAA
Makao Makuu; Enhe, huyo Msaga Sumu amepanda au nini kinaendelea sasa we Andrew? Andrew: Mkuu sasa hivi ni zamu ya huyu chipukizi anayekuja kwa kasi ndani ya Bongo Fleva, Staric anafanya yake jukwaani. Anaimba wimbo wa mwisho. Saa 5: 35 usiku

DIAMOND ATINGA UKUMBINI
Makao Makuu: Deogratius upo wapi mbona husomeki? Deogratius: Mkuu nilikuwa huku getini, namuona Diamond anaingia na mabaunsa wake, full mbwembwe. Saa 5:40 usiku

MSAGA SUMU AKINUKISHA
Makao Makuu: Mayasa upo? Mayasa: Mkuu nipo, hapa namuona Msaga Sumu anamalizia shoo yake. Watu wanashangilia kweli zile ngoma zake za uswahilini. Wanaimba na kucheza naye pamoja. Anataka kushuka lakini mashabiki wanagoma, wanataka aendelee. Makao Makuu: Hao nawajua, Msaga Sumu na Mbagala tena, hapo panachimbika sasa hivi. Saa 5: 50 usiku

DIAMOND APANDA JUKWAANI Mayasa:
Mkuu hatimaye Diamond anakuja jukwaani. Ameanza na wimbo
wa Nataka Kulewa, shangwe la hatari. Yani hapa ni shiiida watu wanagombania kuja kumshika mkono. Burudani ndiyo kwanza inaanza. Makao Makuu: Natamani na mimi ningekuwepo ukumbini niinjoi kidogo! Mayasa: Tayari wimbo wa kwanza umeisha, sasa anaimba wimbo wa Kizaizai, ni balaa. Watu wanapiga kelele kwelikweli. Wengine wanamfuatisha, yani hapa ni burudani kwa kweli. Saa 6:20 usiku

ZARI AWA GUMZO
Makao Makuu: Musa vipi upo humo ukumbini au umesinzia? Musa: Nipo bosi wangu. Hapa sasa hivi Zari amekuwa gumzo wakati Diamond akiimba wimbo wa Mawazo, watu wanapiga kelele ‘Zarii..Zarii...Zariii. Nahisi wanatamani angekuwepo ampe kampani mpenzi wake jukwaani. Makao Makuu: Hahaha! Hao nao wana ‘mahaba’. Hawajamuulizia yule wa zamani? Nanilii... Sepetunga? Musa: Hahah Mkuu uchokozi huo, mimi simo. Kifupi hapa ni bandika bandua, Diamond hana mpinzani Bongo aise. Ukumbi umejaa sijawahi kuona. Shoo hii ya leo amevuja rekodi ya shoo ile ya mwaka jana. Huwezi amini, watu nasiki wameshindwa kuingia maana ndani kumefurika. Makao Makuu: Huyo ndiyo Diamond, endeleeni kufuatilia kila kitu. Najua hapo ni burudani. Malizieni shoo, tukutane asubuhi ofi sini.

MKE WA MOSE IYOBO AIBUKA
Mayasa: Mkuu mbona unatuaga harakaharaka, huku namuona mke wa Mose Iyobo mzazi mwenzie na Aunt Ezekiel kaibuka nadhani kaja kumchunga mumewe asichepuke. Makao Makuu: Hahaha, sasa atakuwa amechelewa sana, amchunge mumewe wakati alishachepuka na kuzaa  nje ya ndoa, hicho si kichekesho, achana naye bwana we nenda kalale tukutane kesho kazini kama kawaida. Mayasa: Sawa bosi usiku mwema.
WAANDISHI WETU
Powered by Blogger.