Diamond, mama’ke kikao kizito ili kupata muafaka wa mpenzi wake!
Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ na mama’ke mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ wamelazimika
kukaa kikao kizito ili kupata muafaka wa mzazi mwenzake na staa huyo,
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurejea Bongo na kuishi katika nyumba
moja na mkwewe huyo ambaye walipishana kauli hivi karibuni.
Hivi karibuni, Zari aliyekuwa akiishi na
mama Diamond nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini Dar, walipishana
kauli na mzazi huyo sambamba na ndugu zake hadi kufikia hatua mrembo
huyo aliyezaa mtoto mmoja na Diamond (Tiffah) kurejea nyumbani kwake
Afrika Kusini kupisha kile alichokiita ni ‘uswahili’.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, baada ya
kuona Diamond anampenda Zari na mapenzi yao ni motomoto, familia haikuwa
na jinsi zaidi ya kukaa kikao kulijadili kwa kirefu suala hilo na
kupata muafaka ambapo habari njema ni kwamba, mama Tiffah anatarajia
kutua Bongo siku chache zijazo.
“Diamond si unajua ndiyo kichwa katika
familia. Amewaita ndugu akawaeleza dhamira na mikakati yake na Zari
hivyo wamekubaliana arejee Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.
“Kila kitu kipo sawa. Zari ataibuka na maisha yataendelea kama kawaida, haya mambo ya kifamilia bwana,” alisema Diamond.
Kabla ya kufikia muafaka huo, Zari
aliripotiwa kuwa anakuja nchini Desemba 8, mwaka huu wakati mama Diamond
akionekana kupinga lakini hatimaye muafaka umepatikana.
CHANZO: GPL

Post a Comment