Rais Magufuli Akutana na Mabolozi Wa China na Korea Kusini...Ahakikishiwa Ujenzi wa Daraja la Salender Dar
Vichwa vya habari za siasa Tanzania bado vinaendelea kubeba stori kila mara kuhusu Rais Magufuli… inawezekana ni kawaida kabisa kila siku kukutana na habari zaidi ya tatu au nne kuhusu Rais Magufuli tangu siku ya kwanza alipoapishwa na kuanza kazi ya Urais wa Tanzania.
Ninayo nyingine kutoka Ikulu sasahivi, hii inahusu Rais Magufuli kumuaga Balozi wa Korea Kusini, Chung IL ambapo Balozi huyo amemhakikishia Rais Magufuli kwamba daraja hilo litajengwa kwa ufadhili wa Serikali yake.
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa
Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, Ikulu jijini Dar es salaam
leo Novemba 30, 2015.
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa
nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.
Post a Comment