Maagizo ya Serikali Kwa Watumishi Wote wa Umma Kuhusu Kwenda Kazini Au Kutoenda Tarehe 9 Disemba Yako Hapa
SERIKALI imesema siku ya Desemba 9 iliyopangwa kuwa siku ya usafi wa mazingingira haitawafanya wafanyakazi wa utumishi wa umma kwenda kazini bali wataungana na wananchi kwenye maeneo wanayoishi kwa kufanya usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa leo
na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es salaam na kusema
kwamba Watumishi wa Umma wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi
katika maeneo yao na yale watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa
wanayoishi.
“Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.
Mkurugenzi amesema
kuwa Watumishi wa Umma hawataenda kazini badala yake watabaki
nyumbani na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo
yanayozunguka mitaa wanayoishi ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro
iliyoziba pamoja na kuzoa taka zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.
Ameongeza
kuwa muongozo kuhusu namna zoezi la usafi litakavyotekelezwa
umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa Uongozi wa Mikoa hadi
Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji tuu wa agizo hilo kwa kila
mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia shughuli nyingine za kila siku
kuhakikisha anafanya usafi.
Aidha
Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila eneo kutengeneza utaratibu mzuri
ambao utafanikisha zoezi la usafi kufanikiwa kwa kuhakikisha
wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya
kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.
Hata
hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru
wa Tanganyika uliopatikana miaka hamsini na nne iliyopita lakini kwa
mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya usafi nchi nzima.
Post a Comment