Lulu awacharukia wanaohoji gharama za urembo wake
STAA asiyekaukiwa matukio Bongo Movies,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacharukia watu wanaohoji kwa nini
anapendeza angali mwanafunzi kwa kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni
mwiko kupendeza?’
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
hivi karibuni, Lulu alisema amekuwa akiona maoni ya watu wengi
mtandaoni wakihoji anapata wapi fedha za kupendeza wakati yeye ni
mwanafunzi hoja ambayo ameiona haina mashiko kwani yeye hatumii fedha
nyingi katika urembo wake.
“Watu bwana! Ningekuwa niko rafu
wangesema pia na hata hivi ninavyopendeza watu wanachonga pia sasa
jamani kipi kitu kizuri ili watu wafurahi na nafsi zao? Mimi umaridadi
hapa ndiyo kwake na sijaanza leo, japo sina fedha lakini kidogo
nilichonacho kinaficha umasikini,” alisema Lulu.

Post a Comment