ad

ad

HADITHI: ... RAHA YENYE MAUMIVU -04


SEHEMU: 04
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
ILIPOISHIA:
Walikwenda hadi chumbani na kukisoma kile cheti kilicho onyesha yupo safi alichopima ANGAZA.
"Sasa itakuwaje?"
"Mwambie humuamini ikiwezekana muende wote."
"Mmh, na tukienda wote na akaonekana yupo safi itakuwaje?"
"Nakuhakikishia hawezi," Eliza alimtia moyo Gift.
"Mmh, nitajaribu."
Waliagana kila mmoja alijiandaa na masomo ya usiku lakini Gift hakuhudhulia aliamua kulala.
SASA ENDELEA…

Asubuhi kama kawaida walikutana Kanuth alimchanulia Gift tabasamu pana
"Ooh, mrembo nina imani amelala njozi tamu zilizo kufanya usisikie uchovu ulipo amka asubuhi."
"Si kweli mawazo yako."
"Nini tatizo?"
"Kwa nini umenidanganya Kanuth kwa kugushi cheti ili uonekane mzima kwa nini unataka kuniua kosa langu nini kwani mapenzi lazima," Gift alianza kuporomosha machozi.
"Nafikiri baada ya muumba ni mimi ninaye yajali maisha yako, kama huniamini tuongozane na wewe mguu kwa mguu popote unapo paamini ili uthibitishe watu hawanitakii mema."
"Kweli upo tayari twende sasa hivi?"
"Nipo tayari popote unapo paamini na daktari unaye muamini ili kuthibitisha nipo safi na nina nia ya kweli na wewe."
Kauli ule ilikuwa kama kisu chenye moto kwenye siagi kwenye moyo wa Gift na kuona huenda yote aliyo sikia ni uongo kwa jinsi kila aliloambiwa na Eliza lilikuwa kinyume.
Alijikuta akimkubalia kwa sharti la penzi lao liwe siri mpaka hapo watakapo maliza shule na kuutangaza uchumba wao kabisa, naye Kanuth alikubali kuilinda siri ya mapenzi kwa kulifanya penzi lao kuwa la siri.
Tokea siku ile Gift na Kanuth walikuwa wapenzi mwanzo kweli lilikuwa penzi la siri, lakini siku zote mapenzi kikohozi kuyaficha huyawezi. Ilikuwa siri mwishowe ikawa bayana kila mmoja alijua penzi la Kanuth na Gift.
Siku zote jasiri haachi asiri siku moja Gift alipigiwa simu na mtu mmoja asiye mjua na kumuomba aende maeneo ya Sinza kwenye hote mpya iliyo karibu na Legho ameonekana Kanuth akiwa na rafiki yake mpenzi kipenzi Eliza.
Presha ikiwa juu alikodi gari hadi kwenye ile hoteli na kwenda moja kwa moja chumba alichoelekezwa, alipofika alitaka kugonga lakini akili nyingine ilimwambia ajaribu kufungua mlango alizungusha kitasa mlango ulitii amri na kufunguka.
Alijitoma ndani, picha aliyoikuta ilimfanya asiamini macho yake alikuwa kweli Kanuth na shoga yake kipenzi Eliza wakivunja amri ya sita. Cha ajabu pamoja na kumwona waliendelea kufanya mchezo wao mchafu bila kuhofu jambo lolote kitu kilicho mfanya Gift kushikwa na kizunguzungu na kuanguka chini nakupoteza fahamu.
****
Gift alipozinduka alijikuta akiwa amelala chini peke yake ndani ya chumba cha guest hapakuwepo Kanuth wala shoga yake Eliza. Alijinyanyua na kukaa kitako akiwaza nini kilichomtokea hapo ndipo kumbukumbu zilipomrudia alianza kulia kilio cha sauti ya chini na kujilaumu kwa kukubali kuwa mpenzi wa mtu aliyemjua tabia zake japo alikuwa hajawahi kumuona, lakini sifa zake pale chuoni zilikuwa mbaya.
Kweli aliamini wanaume wana lugha tamu za ushawishi ambazo huwa kama kisu cha moto kwenye bonge la mafuta ambacho hukata bila tabu wala kutumia nguvu. Pamoja na kweli Kanuth kuwa malaya wa kiume kilichomuuma ni ile hali ya kumkuta na shoga yake ambaye alimsisitiza asimkubali kuwa mpenzi wa Kanuth kwa kusema huenda ni muathirika wa UKIMWI, lakini ajabu ni yeye huyohuyo amemkuta akiwa na huyo aliyemwita muathirika.
Alijikuta akijishangaa kuendelea kuwepo pale tena kuendelea kulia ni heri aondoke ili arudi chuoni kuliko kuendelea kuwepo pale. Alijinyanyua pale chini ili aondoke mule ndani ya chumba cha nyumba ya wageni.
Gift alitoka ndani ya guet ya Rombo akiwa amechanganyikiwa alikuwa akitembea lakini hakuwa yeye, alijiuliza ni nani aliyempigia simu na alikuwa na maana gani kumpigia simu ile. Bila kujielewa alijikuta akitembea katikati ya barabara bila kujua kama yupo katikati barabara.
Agustino Tamilway a.k.a "Tell me why" akiwa katika mwendo wa kasi huku akiongea na simu yake kiganjani katika maongezi ambayo yalimfanya akili yake ihamie kwenye maongezi ndani ya simu.
Aliponyanyua macho hamadi! Mbele yake alikuwepo msichana ambaye alionyesha wazi amechanganyikiwa. Alijikuta akitumia uwezo wake wote kumkwepa yule msichana ambaye alionekana amechanganyikiwa. Alijikuta anafunga breki huku akiuma meno mpaka tairi za gali zilinuka kwa kujiburuza.
Alifanikiwa kufunga breki lakini gari liliseleleka kutokana na mwendo makali na kumpiga kikumbo Gift na kumtupa mbali kidogo. Tell me why alitereka kwenye gari na kumkimbilia Gift ambaye alikuwa ameanguka chini damu zikimtoka kichwani na alikuwa amepoteza fahamu.
Alimchukuwa harakaharaka kabla watu hawajakuwa wengi na kumuingiza kwenye gari lake, kwa haraka aligeuza gari na kumwahisha hospitali ya TMJ iliyopo Mikoche ambayo ndiyo anayotibiwa yeye. Alipomfikisha harakaharaka alichukuliwa na wauguzi na kukimbiziwa hodini tayari kwa huduma.
Tell me Why alikutana na daktali Eliud na kumwelezea sababu ya ajali
"Ina maana mgonjwa hakuwa na jamaa au ndugu?" Dakta aliuliza.
"Kwa kweli sijui kwa sababu baada ya kujitahidi kumkwepa na kukumba na bodi ya gari nilichojua ni kumwahisha hospitali ili kuokoa maisha yake zaidi ya hapo sijui."
"Pole sana, ni hali ya kawaida ambayo huwakuta watu wengi lakini wewe umeonyesha moyo wa ujasiri na huruma, mara nyingi watu wanapotokewa na tukio kama hili hukimbia na kumwacha mgonjwa bila kujua nini hatma yake.”
"Unajua nini Mr Eliud mara nyingi sababu ya madereva kukimbia husababishwa na wananchi wanaojiita raia wenye hasira kali, wao wanachojua kila ajali ni uzembe wa dereva. Baada ya ajali humuangushia kipigo dereva bila kujua ni yeye huyo mwenye usafiri anayeweza kuokoa maisha ya huyo mgonjwa kwa kumuwahisha hospitali."
"Ni kweli lakini nimegundua wengi ni wezi ambao hutumia nafasi ile kumuibia dereva chochote kilichomo kwenye gari...Sasa Mr Tell me why wacha nimshughulikie mgonjwa kwa sababu nimewaachia kazi ya kuchukua vipimo vya awali ili kujua ameumia kwa kiasi gani."
Dakta Eliud alikwenda kumuangalia mgonjwa na kuangalia vipimo, na kumuacha Mr Tell me why akiwa amejiinamia kwa mawazo na kujiuliza maswali mengi juu ya mgonjwa na hali yake. Alijikuta akijiuliza alikuwa anatoka wapi na kwa nini alikuwa akitembea katikati ya barabara ilionyesha alikuwa amechanganyikiwa.
Alimuomba Mungu amponyeshe upesi na majeraha yake yasiwe makubwa aliamini kikumbo kilichompata huenda maumivu yake yasiwe makubwa sana. Akiwa ameinama alishtushwa na sauti ya Dakta Eliud
"Mr tell me..vipi naona tukio limekuchanganya sana?"
Sauti ile ilimfanya anyanyuke kwa haraka kutaka kujua hali ya mgonjwa.
"Vipi Doctor hali ya mgonjwa ikoje?"
" Tuliza munkali Mr."
"Dakta ni vigumu kutulia kutoka roho ya mtu bila kutegemea lazima uchanganyikiwe...Vipi hali yake?"
"Tuliza munkali hali ya mgonjwa sio mbaya."
"Ooh, asante Mungu ningekuwa mgeni wa nani kibaya zaidi hata ndugu zake siwajui."
"Ila..."
"Oooh doctor ila nini tena?"
"Punguza munkali Mr tell me, kila kitu kitakuwa sawa ila nilitaka kukueleza kuwa hali yake si mbaya ni majeraha madogo siyo makubwa ya kutisha japo la kichwani ni kubwa kidogo lakini halihitaji kushonwa bali kufungwa dawa tu."
"Ooh afadhali," Mr Tell me why alishusha pumzi ndefu kisha alisema.
"Mr Eliud naweza kwenda kumuona mgonjwa wangu?"
"Mmh mara hii ameisha kuwa mgonjwa wako wakati umemuokota njiani?"
"Hapana kwa sasa ni mgonjwa wangu mpaka hapo nitakapo mkabidhi kwa familia yake."

Nini Kitaendelea? Ili kuyajua yote endelea kufuatulia.
Powered by Blogger.