Singidani (A Story From My Heart) - 15

ILIPOISHIA…
Aliporudisha macho yake barabarani, alishangazwa sana na kitu kilichotokea!
“Nakufaaa…” Laura akapiga kelele.
SASA ENDELEA…
Aliporudisha macho yake barabarani, alishangazwa sana na kitu kilichotokea!
“Nakufaaa…” Laura akapiga kelele.
SASA ENDELEA…
UZURI wa Laura ulikuwa tishio,
dereva alishachanganywa na uzuri wa Laura. Pamoja na urembo wa sura yake,
hakuweza kuficha ushamba wake wa jiji kubwa la Dar es Salaam. Ingawa alikuwa na
ndugu zake, lakini hakuwa akienda Dar mara kwa mara.
Macho ya kuangaza kila mahali,
hakuweza kuyaepuka! Ni sababu hiyo ndiyo ilimfanya dereva achanganyikiwe na
kutokuwa makini barabarani. Gari lilikuwa mbele yake kwenye mataa ya Shekilango
hakuliona. Aliliona likiwa mita chache sana mbele yake.
Alifunga breki kwa nguvu... Laura
akafumba macho ili asishuhudie ile ajali. Kwa bahati nzuri, akiwa anakaribia
kabisa kuligonga lile gari, tayari magari yalishaanza kutembea... taa ya kijani
ilishawaka! Hiyo ndiyo ikawa salama yao!
Taratibu wakateleza. Laura alifumbua
macho, akahema kwa kasi sana.
“Weweee jamaniiii!” akasema kwa sauti dhaifu, akijaribu kuvuta pumzi ndefu sana...
Akazishusha taratibu kabisa!
“Kumbe wewe mwoga sana?” dereva yule akasema, safari hii akiwa makini sana barabarani.
“Kwani we huogopi?”

“Naogopa pia... lakini usijali.
Tatizo ni wewe bwana!”
“Tatizo mimi, kivipi?”
“Tuachane na hayo, kuhusu hawa jamaa wa Bongo Movies, ukitaka kuwapata kwa urahisi ni Jumamosi mara nyingi wanakutana Leaders Club.”
“Tatizo mimi, kivipi?”
“Tuachane na hayo, kuhusu hawa jamaa wa Bongo Movies, ukitaka kuwapata kwa urahisi ni Jumamosi mara nyingi wanakutana Leaders Club.”
“Kinondoni?”
“Ndiyo.”
“Huwa wanafanya nini hapo?”
“Si unajua tena mambo ya wasanii, wanakutana na kujadiliana mambo yao tu. Kiukweli sijui mambo yao vizuri zaidi ya hapo.”
“Ndiyo.”
“Huwa wanafanya nini hapo?”
“Si unajua tena mambo ya wasanii, wanakutana na kujadiliana mambo yao tu. Kiukweli sijui mambo yao vizuri zaidi ya hapo.”
“Ahsante, najua nitaweza kuanzia
hapo. Ingia hapo kushoto, nataka kushukia hapo Tip Top.”
“Barabarani kabisa au unataka nikuingize ndani?”
“Hapana, hapo barabarani tu panatosha kabisa.”
Dereva akapinda kushoto na kuegesha nyuma kidogo ya kituo cha daladala, Tip Top. Laura akamlipa yule dereva na kubaki hapo amesimama kwa muda. Dereva akaondoa gari.

Laura aliangaza macho huku na huko,
kisha akaamua kuifuata barabara ya vumbi iliyokuwa ikielekea Manzese – Uzuri.
Alitembea taratibu kwa mtindo wa kuangaza huko na huko. Mbele kidogo akaona
bango dogo juu ya nyumba limeandikwa Waridi Lodge.
Laura akatabasamu. Akaenda mpaka
hapo, akapita moja kwa moja Mapokezi. Akapokelewa na dada mrembo sana, lakini
alijihakikishia kuwa, pamoja na urembo wa dada huyo, bado hakufua dafu mbele
yake! Yeye alikuwa mzuri kuliko huyo msichana!
“Nahitaji chumba,” akasema Laura.
“Umepata mrembo!”
Laura akaandikisha kwenye kitabu cha wageni. Kisha akepelekwa kwenye chumba chake.
“Nahitaji chumba,” akasema Laura.
“Umepata mrembo!”
Laura akaandikisha kwenye kitabu cha wageni. Kisha akepelekwa kwenye chumba chake.
***
Ilikuwa Jumamosi, wasanii wengi wa filamu walikuwa wamekaa kwenye viti vya plastiki, pembeni mwa uwanja wa mpira wa pete katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Eneo karibu lote lilikuwa na watu wengi sana.
Mapema sana!
Saa tano asubuhi!

Supu ilinywewa kwa fujo, wengine
nyama choma na bia. Kifupi watu walikuwa kwenye mapumziko ya mwisho wa wiki.
Wengi wa wasanii wale walikuwa ni wanachama wa klabu yao ya Bongo Film. Wasanii
wa klabu hiyo hukutana hapo kila Jumamosi kwa ajili ya kuweka mikakati yao ya
kisanii.
Ilibaki nusu saa tu kikao rasmi kianze.
Ilibaki nusu saa tu kikao rasmi kianze.
***
Aliteremsha mguu wa kwanza chini kutoka kwenye gari alilokuwa amepanda. Kisha ukafuata mwingine. Baadaye, mwili mzima ulitoka ndani ya gari. Akasimama na kusukuma mlango kwa nguvu wa gari kwa nguvu. Akapunga mkono kumuaga dereva, ambaye aligeuza gari na kuondoka.

Alikuwa msichana mrembo kuliko
kawaida. Namna yake ya kutembea ikawa kivutio kingine kwa watu waliokuwa
wakimtazama wakati akitembea kwa madaha. Macho yote yalikuwa kwake. Si wanaume
wala wanawake.
Wote walishangazwa na uzuri wa
msichana yule. Kwa alivyoonekana alijua alichokuwa akikifanya. Alijua alipokuwa
anakwenda na alimjua aliyekuwa akimfuata. Alinyoosha moja kwa moja hadi
walipokuwa wamekaa wasanii wa filamu.
Wasanii wote wakapagawishwa na uzuri
wake. Akasimama katikati yao, akawaangalia kwa zamu, kisha akavua miwani yake
myeusi iliyokuwa usoni mwake. Macho yake mazuri yakawa tatizo lingine!
“Samahanini jamani... samahani sana ndugu zangu. Nimekuja hapa kwa sababu ya mtu mmoja tu; Chris!” akasema msichana yule.
Alikuwa ni Laura.
“Samahanini jamani... samahani sana ndugu zangu. Nimekuja hapa kwa sababu ya mtu mmoja tu; Chris!” akasema msichana yule.
Alikuwa ni Laura.
Dk. Chris alishtuka sana alipomuona
Laura eneo lile. Akasimama na kumwangalia kwa hasira.
“Kaa mbali kabisa na maisha yangu. Sitaki matatizo. Kama umetumwa, mnajidanganya, mimi ni daktari kitaaluma, tena nimesoma nje ya nchi, mimi siyo bwege!” alisema Dk. Chris kwa hasira.
Itaendelea
“Kaa mbali kabisa na maisha yangu. Sitaki matatizo. Kama umetumwa, mnajidanganya, mimi ni daktari kitaaluma, tena nimesoma nje ya nchi, mimi siyo bwege!” alisema Dk. Chris kwa hasira.
Post a Comment