Masogange afungukia penzi la Davido
Video Queen mwenye umbo tata Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’.
VIDEO Queen mwenye umbo tata Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’ alifungukia penzi lake na staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido.
Akizungumza na Amani Masogange
alisema kuwa kuna uvumi unaovumishwa na baadhi ya watu kwamba amekuwa
akitoka kimalovee na Davido jambo ambalo halina ukweli wowote.
“Kwanza kabisa Davido ni shemeji yangu lakini pia kuna ‘project’ kubwa ambayo tunaiandaa. Mtakuja kuelewa tu hapo mbeleni na si jambo la kusema ni wapenzi bila kuthibitisha,” alisema Masogange.
CHANZO: GPL

Post a Comment