Rayuu, Skaina wafanya uchafu
Mastaa wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ pamoja na Skyner Ally ‘Skaina’.
Mayasa Mariwata
MASTAA wa
filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ pamoja na Skyner Ally ‘Skaina’
wanadaiwa kufanya uchafu baada ya picha za wawili hao wakionesha mahaba
hadharani kusambaa.
Chanzo kinaanika kuwa wawili hao hivi
karibuni walikutana katika Ukumbi wa KD, Kijitonyama ambapo kulikuwa na
sherehe ya kuzaliwa kwa Rayuu huku wakionesha mahaba ya mtu na mpenzi
wake ndipo picha hizo zilipopatikana.
Baada ya madai haya, Amani lilimvutia waya Skaina ambapo simu yake haikuwepo hewani lakini lilipomtafuta Rayuu alisema kuwa haoni kama kuna cha ajabu.
“Sina tabia chafu, yale yalikuwa ni
mambo ya Kizungu tu maana ilikuwa bethidei na mwenyewe (Skaina) katika
kipindi cha kulishana keki aliamua kutumia mdomo,” alisema Rayuu.
CHANZO: GPL

Post a Comment