MAGUFULI AAHIDI NEEMA SINGIDA, LEO KUIANZA KONDOA
Magufuli akiongea na umati uliofurika katika kijiji cha Nduguti, Jimbo la Iramba mashariki.
Akizungumza na wakazi mbalimbali kwenye maeneo aliyofanya mikutano ya leo Magufuli aliwaahidi vijana kupata ajira katika serikali yake kupitia sera yake ya uanzishaji viwanda pamoja na kutoa ajira serikalini bila upendeleo wala visingizio vya uzoefu kazini.
Magufuli aliwalaumu viongozi wenye tabia ya kuwawekea kauzibe vijana wanaotoka masomoni na kuwaambia hawawezi kuajiriwa mpaka wawe na uzoefu kazini jambo ambalo linawakwamisha wasomi wengi wanaotoka masomoni.
Amesema katika utawala wake ukitoka masomoni unafikia ajira ilimradi uweze kuimudu.
Pamoja na ajira kwa vijana Magufuli aliwaahidi wakazi wa vijiji alivyotembelea kuwa atazidi kusambaza umeme katika vijiji ambavyo haujafika na kutatua tatizo la maji mkoani humo ambalo lilishaanza kutatuliwa na uongozi uliopita lakini yeye ataboresha zaidi suala hilo.
Kila alipotembelea mgombea huyo alishangiliwa na umati wa watu wa vyama mbalimbali hasa alipotangaza ilani ya chama chake ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na pale alipotangaza serikali yake ikiingia madarakani kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama na vijana kwa kila kijiji na kila kata nchi nzima.
Magombea huyo pia alisema serikali ya chama chake juzi Alhamisi kimepokea msaada wa shilingi bilioni 992 kutoka Marekani kwa ajili ya miradi ya maendeleo hivyo wananchi wakae mkao wa neema endapo atachaguliwa kuingia ikulu.
Mwisho Magufuli aliwaasa wakazi wa Singida kutoichezea bahati hiyo kwa kuwachangua viongozi wa vyama vya upinzani na kuataka wamchague kwenye urais na kuwapa ubunge wagombea wa CCM na Madiwani.
(Habari Picha:Richard Bukos)
Post a Comment