Ujauzito wamtuliza amanda
Staa wa filamu za Kibongo, Amanda Poshy.
STAA wa filamu za Kibongo, Amanda Posh anadaiwa kutulizwa na hali yake ya ujauzito kwani hivi sasa haonekani mara kwa mara kama zamani.
Chanzo kilicho karibu na muigizaji huyo kilisema Amanda alikwenda nchini Uswisi ambako ndiko anakoishi mpenzi wake, ambaye hata hivyo jina lake halikupatikana mara moja, aliporejea ndipo ilipojulikana ni mjamzito.
Amanda alitafutwa na gazeti hili ili kuthibitisha kama kweli ‘kitu’ kimeitika, naye akajibu kwa kifupi; “Kwani tatizo liko wapi wakati mimi ni mwanamke, kuna ajabu gani nikiwa na mimba? Mmeshaanza umbeya wenu.”


Post a Comment