ad

ad

SIRI DK. SLAA KWENDA KUISHI MAREKANI ZIPO HAPA...amekwenda kimkakati,

 
Na Neophitius Kyaruzi

UAMUZI wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa (pichani) kwenda kuishi Marekani kwa muda usiojulikana  haukutokana na utashi binafsi bali  una siri nzito nyuma yake,  Uwazi Mizengwe limefahamishwa. Taarifa kutoka kwa vyanzo vya uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zimedai kuwa,  Dk. Slaa amekwenda nchini humo kimkakati, kupitia nyaraka mbalimbali za Chadema na kuandaa ripoti iliyosheheni kashfa za kiutendaji ili itumike kukisambaratisha chama hicho kabla na baada ya uchaguzi mkuu ujao. “Dk. Slaa amekwenda Marekani kwa kazi maalum ya kuandaa ripoti kuhusu siri na kashfa mbalimbali ndani ya Chadema ikiwamo mfumo wa upatikanaji nyaraka za serikali, matumizi mabaya ya fedha za ruzuku, mikakati ya muda  wa kati na mrefu wa kuimarisha upinzani dhidi ya CCM na kashfa za kifisadi ndani ya chama hicho ili kuhakikisha kwamba kinasambaratika,” kilisema chanzo chetu. Wakati taarifa hiyo ikivuja hivyo, hivi karibuni mwanasiasa huyo ambaye awali alitangaza kuachana na siasa zinazofungamana na vyama, alitumia fursa ya mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Azam kuwaaga Watanzania huku akiahidi kurejea nchini kwa muda usiojulikana. Hata hivyo, alisisitiza kwamba siku akirejea atatoa ‘silaha’ nzito
alizozihifadhi kusubiri wakati ufike.

 SABABU YA KULINDWA NA USALAMA WA TAIFA Taarifa zinasema kwamba kutokana na unyeti wa kazi hiyo, usalama wake ulikuwa hatarini kwa kuwa amekuwa katibu mkuu wa Chadema
kwa kipindi kirefu hivyo anajua siri nyingi za chama iwapo akizitoa kwa
CCM yatatokea ‘maafa’ makubwa ndani ya chama hicho ikiwamo kuvunjika vipande vipande. Chanzo chetu kilisema kwamba kutokana na unyeti wa taarifa hizo ambazo zinaweza kudhoofisha au kuua upinzani nchini, hali ya usalama ya mwanasiasa huyo ilikuwa hatarini ndiyo maana tangu alipoamua kuanza kutoboa siri, alipewa ulinzi mkali na idara ya usalama wa taifa. Dk. Slaa alikiri kulindwa na idara hiyo akiwa nchini huku akisisitiza kuwa bila hivyo maisha yake yalikuwa hatarini.


 KUIMARISHIWA ULINZI MAREKANI 
Taarifa zaidi zinasema kuwa, akiwa nchini Marekani, Dk. Slaa ataendelea kuimarishiwa ulinzi kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa uhakika na hatimaye iweze kutekelezeka kama ilivyopangwa.   Imeelezwa kwamba, taarifa atakayoiandaa ina masilahi makubwa kwa taifa kwani itaibua masuala mazito ya ufisadi mkubwa ambao umekuwa ukifanywa na viongozi mbalimbali hasa waliohamia Chadema kutaka kuficha madhambi yao kwa kigezo cha kuungwa mkono na wananchi ambao hawajui undani wa kashfa zinazowakabili.

ADAIWA KUDANGANYA ILI ASIFUATILIWE
Chanzo hicho kilidai kuwa, Dk. Slaa kwa makusudi aliwadanganya Watanzania wakati akiaga kuwa anakwenda kujiendeleza kimasomo,
huku akisisitiza: “Nakwenda kujinoa zaidi katika lugha ambazo nimeanza kuzisahau.” Alidai kutaka kujikumbusha masomo ya sheria na theolojia lakini bila kufafanua sababu za kufanya hivyo. Ilielezwa kuwa alitoa ufafanuzi huo ili asiweze kufuatiliwa, kwani kama angepotea ghafla, wabaya wake wangeweza kumfuatilia mahali alipo na kutaka kujua anachokifanya na malengo yake.

UKIMYA WA SIKU KADHAA BILA KUJITOKEZA Taarifa za uhakika zilizotufikia zinaeleza kuwa, Dk. Slaa si kwamba kipindi alichokuwa kimya, alikuwa akitafakari nini cha kufanya bali alikuwa katika mashauriano mazito  na kundi linalomuunga mkono katika mkakati huo wa sasa, hivyo baada ya mipango yote kukamilika ndipo alipoamua kujitokeza hadharani ili kuzungumzia mikakati yake ambayo ndiyo kwanza imeanza kutekelezwa.

GHARAMA ZA ‘PROJECT’ NZIMA Kwa mujibu wa chanzo hicho, kundi linalomuunga mkono (halitajwi kwa jina) ndilo lililomfadhili kutekeleza kazi hiyo kwani kuna mkataba mzito kati yao kuhakikisha kuwa, kazi hiyo inafanyika kwa ufasaha. Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kiasi maalum cha fedha kilichoelezwa ingawa chanzo kinadai kuwa ataendelea kumwagiwa fedha za kumwezesha kuishi Marekani na kumudu gharama nyingine za kazi hiyo hadi hapo itakapokamilika.


CHANZO: UWAZI MIZENGWE
Powered by Blogger.