Sajenti, siasa na malezi ya mtoto wapi na wapi?
MAISHA ya
Kibongo kwa kweli ni magumu sana. Kuna msemo mmoja maarufu sana mtaani
unaosema kuwa bora jana kuliko leo, wakimaanisha angalau jana walikuwa
na uhakika, hawajui leo itakuwaje.
Vijana
wako bize kutafuta hela kwa kila mbinu, wenye haraka wakitumia silaha,
ushirikina na hata utapeli, ili mradi kila mmoja anajitahidi kuhakikisha
maisha yake ya leo yanakwenda sawa, huku akijiweka vizuri kuishika
kesho yake isiingie mushkeli.
Husna
Sajenti ambaye ni muigizaji wa filamu Bongo, ambaye ni mzazi mwenzie na
mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ ni
miongoni mwa vijana hao wa Kibongo ambao wako bize kuhakikisha fedha
zinaingia ili maisha yaendelee, no matter what!
Habari
njema kwa mashabiki wa Husna ni kwamba wiki chache zilizopita, binti
huyo alijifungua mtoto wake wa pili (huyu hakuzaa na Chaz Baba) na hivyo
kuzidi kuongeza idadi ya wanafamilia yake. Kwa jamii nyingi za
Kiafrika, licha ya kiuchumi kujiongezea mzigo, lakini ujio wa kiumbe
kipya katika familia ni jambo la kupongezwa!
Ingawa
hata hivyo, maisha ya mtu ni yake binafsi, wakati mwingine siyo jambo
baya kumshauri unapoona anachokifanya, ama hakiendi sawa kijamii, kiafya
au hata kiutamaduni.
Akiwa
na wiki moja tu tangu ajifungue, Husna ameonekana mara kadhaa akiwa
katika matukio ya kisiasa yanayofanyika usiku, lakini akiwa peke yake.
Maana yake ni kuwa mwanaye mchanga, humuacha peke yake nyumbani, au
huenda naye na kumkabidhi mtu mwingine anayekuwa mbali na alipokaa.
Ni
kweli kuwa katika maisha ya uzungu ambayo vijana wengi wa Kiafrika
wanajaribu kuishi, hili ni jambo la kisasa, tofauti na mama zetu ambao
mila ziliwalazimisha kuamini kuwa mtoto hawezi kuachwa peke yake hadi
amalize siku 40 tangu azaliwe!
Na
upo ushahidi wa mazingira kuwa wasanii wanaojitokeza katika mikusanyiko
ya vyama vya siasa vilivyo katika kampeni hivi sasa, wanalipwa. Yes, ni
wakati huu wa kuchangamka, kwa sababu usipotumia nafasi yako,
utachekwa!
Hata
hivyo, pamoja na uchu wetu wa fedha, sidhani kama ni jambo jema kwa
afya ya mtoto, tena wa Kiafrika, mama mzazi kwenda kwenye matukio ya
usiku na kukaa huko hadi majogoo!
Na
huenda hayo ni matukio ambayo tunamuona, kwa sababu hata sisi pia
huwepo huko. Kama ishu ni kwa sababu ya mkwanja, kwamba analipwa
sifikiri kama hakuna maeneo mengine yenye fedha yanayoweza kumvutia na
kwenda nyakati za usiku!
Kama
hivi ndivyo, nadhani dada huyu anahitaji ushauri kidogo, kwa namna ya
kumkumbusha kuwa kila kitu na wakati wake, ndiyo maana kuna muda wa
kibaolojia ambao mwanamke anabeba mimba.
Vivyo
hivyo, anao muda anaopaswa kumlea kwa karibu mwanaye, kwani tunajua
ataacha kunyonya, ataanza kutembea kabla ya kuanza kujitegemea.
Kumuacha
mtoto katika kipindi ambacho anahitaji joto la mama kwa ukaribu ni
kumnyima haki yake. Kama ishu ni hela, mbona zipo tu maana alizikuta na
ataziacha. Kama zimekuja kipindi ambacho yeye yupo katika malezi, ni
kumshukuru Mungu tu kwani kila mtu na riziki yake inayokuja kwa wakati
wake.

Post a Comment